DIWANI MAFIGA AWATAKA WANANCHI WA KATA HIYO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI.
Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, (kulia) akikagua ujenzi wa madarasa katika shule za Msingi na Sekondari.
Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile,(kushoto) akizungumza jambo na mwalimu wa shule ya Sekondari Mafiga mara baada ya kuwasili katika ukaguzi wa ujenzi wa madarasa.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Misufini ""B"
Ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Mafiga A.
Ujenzi wa madarasa Sekondari Mafiga.
Ujenzi wa Uzio shule ya Msingi Misufini A.
Jengo la Utawala Shule ya Sekondari Mafiga.
Maabara Shule ya Sekondari Mafiga.
Diwani wa Kata ya Mafiga. Mhe. Thomas Butabile, akionyesha Uzio wa ukuta wa Shule ya Msingi Misufini A ambao umeshajengwa na hatua iliyobakia ni kuweka geti.
Jengo la Ofisi ya Kata.
DIWANI wa Kata ya Mafiga, Manispaa ya Morogoro Mhe. Thomas Butabile, amewataka Wananchi wa Kata ya Mafiga kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa.
Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 08/2021 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwamo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika Kata hiyo.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Mafiga A na B, Shule ya Msingi Misufini A na B pamoja na shule ya Sekondari ya Mafiga , Mhe. Butabile, amesema ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na huku akipongeza jitihada hizo za wananchi wa Kata ya Mafiga kwa michango yao ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.Butabile, amesema ni wakati sasa Wananchi wa Kata ya Mafiga kuendelea Kutambua kazi na mchango mkubwa unaofanywa na Serikali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Aidha, Butabile, ameomba Ofisi ya Mnaispaa ya Morogoro kuangalia kwa jicho la tatu Shule ya Sekondari Mafiga kwa ajili ya kuwekwa uzio ili kuweza kudhibiti utoro shuleni pamoja na vibaka wanaopita kwani eneo hilo la shule lipo barabarani .
Katika hatua nyengie, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla lukuba kwa jinsi anavyoweza kuchukua hatua za kuweza kuziingizia Kata fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wa mwananchi wa Kata hiyo, Rajabu Ramadhani Omary, amempongeza Diwani wa Kata hiyo kwa jitihada zake za dhati za kuwasogezea huduma za maendeleo wananchi wa Kata hiyo ikiwamo mazingira rafiki ya wananfunzi kuweza kujisomea.
“Tuna mshukuru sana Diwani wetu wa Kata ya Mafiga , Mhe. Thomas Butabile, kwa kweli amekuwa karibu sana na sisi katika kila jambo, lakini kikubwa zaidi ameonyesha ni jinsi gani Serikali ilivyokuwa makini kwa kuwashirikisha wnanachi kwa mambo muhimu yote yanayohusu maendeleo ya Kata yetu, amekuwa muhamasihaji mzuri sana hususani katika michango ya ujenzi wa madarasa, tunaamini kama wananchi tukiendelea kumpa ushirikiano pamoja na Ofisi ya Kata tutafika mbali na kutoka hapa tulipo, kwa muda mfupi ndani ya siku 60 tumeona ni jinsi gani ana maono makubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo" Amesema Rajabu.
Hata hivyo, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba kwa kuibadilisha Manispaa ya Morogoro kwa kipindi cha muda mfupi katika uongozi wake.
" Huyu mwana mama shupavu sana, tunaona sasa Manispaa yetu imebadilika, huu mji ulikuwa finyu sana , lakini sasa tunaona maendeleo makubwa ukiangalia kuanzia katikati ya Mji pamependeza sana, miradi inaonekana , kwahiyo tunamuombea kwa Mungu azidi kumpa maisha marefu na kumuweka zaidi Manispaa ili azidi kufanya makubwa zaidi ya haya ambayo anayafanya kwa sasa" Ameongeza Rajabu.
Aidha, ameiomba Mamlaka inayosimamia usafiri kuhakikisha kwamba Magari yote yanaingia Stendi ya Mafiga kwani sasa kumezuka viforeni visvyo na msingi eneo la masika jambo ambalo ni kero kubwa kwa watumiaji wa barabara ile hali ipo Stendi kubwa ya Kisasa iliyo bora kabisa katika Mkoa wa Morogoro na nje ya Mkoa.
Miongoni mwa shule zilizotembelewa na Mhe. Diwani ni pamoja na Shule ya Sekondari Mafiga yenye ujenzi wa madarasa 3 yaliyopo hatua za msingi, Shule ya Msingi Mafiga A ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya Mwalimu, Shule ya Msingi Misufini B ujenzi wa madarasa 3 na Ofisi 1 ya mwalimu, Shule ya Msingi Misufini A ujenzi wa Uzio na ukarabati wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa Ofisi ya Kata na Ujenzi wa Tenki la Maji lililofadhiliwa na Taasisi ya Islamic Foundation.
Post a Comment