MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO AAHIDI KUTATUA KERO KICHEFUCHEFU NDANI YA MANISPAA.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amewahakikishia wananchi wa Manispaa ya Morogoro kua hakutakua na kero babaifu za huduma za jamii kutokana na kuwepo kwa mikakati madhubuti iliyowekwa na halmashauri hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
Ameyasema hayo Kupitia kikao cha Kawaida cha
Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya
Manispaa Februari 08/2023.
Kupitia maswali yalioluizwa ya papo kwa papo na Madiwani
wakipambania utatuzi wa changamoto zinazozikabili kata zao,Machela, amewatoa hofu Madiwani
kwa kusema kuwa Manispaa ina mipango mizuri na utekelezaji utaanza mara
moja kwakua fedha za halmashauri zipo za kutosha.
Katika upande wa elimu , Machela, amewataka wananchi kuendelea kujitolea na
kufanikisha upatikanaji wa maboma kwa ajili ya Madarasa na Serikali itamalizia
kwa sehemu iliyobaki kwa asilimia miamoja ikiwa ni pamoja uezekaji na
upatikanaji wa madawati.
Pia amewahakikishia kua swala la upungufu Madawati
linakwenda kuisha hivi karibuni kwakua ni kipaumbele cha kwanza katika bajeti ya
robo ya tatu inayoanza hivi karibuni, jumla ya shilingi 500 zimetengwa kwa
ajili ya Madawati.
Kuhusu huduma
ya afya, Machela, amesema mpango uliokuwepo ni kuhakikisha wanajenga
majengo mawili makubwa ya Upasuaji katika Kituo
cha afya Mafiga na Sabasaba.
“Tutaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi
wetu, mkakati wetu ni ujenzi wa majengo ya upasuaji, lakini suala la changamoto
ya vifaa tiba katika Zahanati zetu, hilo tumeliona na Manispaa imetenga fedha
kidogo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa ambapo hivi karibuni tutaanza
kusambaza huku tukisubiria vifaa vingine toka serikali kuu ambayo ndio
ina dhamana ya kusambaza vifaa tiba baada ya Halmashauri kukamilisha ujenzi wa
Zahanati ” Amesema Machela.
Akijibu hoja ya sintofahamu waliyonayo wananchi wa
Kiegea kuhusu hatma ya umilki wa ardhi, amesema Baraza la Madiwani limepitisha ya kwamba kwa wananchi walioongezewa maeneo
wasitozwe pesa yoyote kwa ongezeko hilo bali wamiliki bure kutokana na uhitaji
wa wananchi wasio na uwezo.
Post a Comment