WAZIRI MABULA AAGIZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUONGEZA NGUVU KATIKA KUKAMILISHA ZOEZI LA URASIMISHAJI.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, ameziagiza mamlaka za Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi nchini kuhakikisha zinaongeza nguvu katika kukamilisha zoezi la urasimishaji wa makazi kabla ya kumalizika kwa mwaka 2023 ambao ndio mwisho wa zoezi hilo.
Waziri Mabula amesema hayo leo Februari 22/2023 katika kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mpango kabambe wa urasimishaji makazi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mabula, amesema kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa inayo jukumu la urasimishaji na upangaji wa miji kwa kushirikiana na Makampuni ya urasimishaji badala ya kuitegemea Wizara kutenga fedha hizo.
" Tumeweka mpango kabambe wa urasimishaji , mwisho mwaka huu 2023, niombe mamlaka za upimaji , usimamizi na uratibu wa ardhi mfanye kazi zenu ipasavyo, niombe mkasimamie vizuri upangaji wa miji ili kuepusha migogoro ya ardhi na kupanga miji vizuri, niwapongeze Manispaa ya Morogoro kwa kufika asilimia 53 ya urasimishaji katika Mkoa wa Morogoro " Amesema Waziri Mabula.
Katika hatua nyengine, amesema maeneo ambayo hayajaendelezwa yanachafua taswira ya Miji na yanapoteza mapato ambayo kama yangeendelezwa yangekuwa na faida kiuchumi, hivyo Viongozi wawaelimishe wananchi kuhusu mipaka ya ardhi pamoja na kuyaendeleza maeneo yao.
Miongoni mwa maagizo aliyotoa kwa Halmashauri nchini ni Halmashauri kukaa na Makapuni waliyoyapa tenda ya kazi ya urasimishaji kukaa nayo ili kuona namna gani gani kazi ambazo hawajakamilisha wanazikamilisha kikamilifu, Kampuni zitakazoshindwa kutekeleza zoezi hilo la urasimishaji wawafutie tenda na kudai fedha zao pamoja na kutokutoa tenda mpya kwa makampuni ambayo hayakumaliza kazi ya urasimishaji.
Dkt. Mabura, amesema , zipo hatua ambazo Wizara ya ardhi imezichukua ikiwemo Wizara kufanya kikao kazi na TAMISEMI kuona namna gani ya kushirikisha Halmashauri kutenga fedha katika Sekta ya ardhi juu ya upangaji na urasimishaji pamoja na kufanya kikao na Makampuni ya urasimishaji ili kuwapa mpango kazi wa utekelezaji wa zoezi la urasmishaji.
Hata hivyo, amesema zipo changamoto ambazo zimejitokeza katika kutofanya vizuri katika mpango kabambe ikiwemo kazi za urasimishaji kuchelewa au kutokukamilika, uchangiaji hafifu wa uchangiaji katika urasimishaji, usimamizi usiolizika kwa mamlaka ya urasimishaji , baadhi ya Makampuni kuchukua pesa bila kumaliza kazi na kutokuwepo kwa kumbukumbu na nyaraka za mapato ya ukusanyaji wa fedha za urasimishaji.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi, Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratias Desderius , amesema asilimia 35 ya wananchi Tanzania wanaishi Mjini huku akisema ongezeko la watu ni asilimia 3.2 .
Amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza nguvu katika upangaji wa maeneo , kwani hali inaonesha zaidi ya miji 4310 imekuwa ikichipuka na kukuwa kutokana na Serikali kuboresha huduma za kijamii Vijijini na Mijini.
Amesema kuwa katika kuona zoezi la urasimishaji linafanikiwa , Wizara imeandaa muongozo wa uendelezaji wa nyumba Vijijini na Makazi bora.
Naye Afisa Mipango Miji Manispaa ya Morogoro, Emeline Kihunrwa, akiwasilisha mpango kabambe wa urasimishaji, amesema asilimia 65 limepimwa na asilimia 35 ya eneo lililopimwa bado barabara zake hazijafunguliwa.
Kihunrwa, ametaja mapendekezo ya mpango kabambe wa Halamshauri , miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuanzisha vituo vya biashara nje ya mji, urasimishaji makazi holela, utunzaji wa vyanzo vya maji, uendelezaji wa mji, kuboresha mifumo ya maji taka na taka ngumu pamoja na kutenge maeneo ya maegesho.
Post a Comment