MANISPAA YA MOROGORO YAMPONGEZA RAIS KUPATA MGAO WA PIKIPIKI
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imenunua pikipiki 916 kwa ajili ya watendaji kata nchini lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa maofisa hao.
Katika pikipiki hizo, Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Halmshauri ambayo imepata pikipiki 1 ambapo Uongozi wa Manispaa umetoa pongezi kwa Mhe. Rais na kuahidi kuitumia ipasavyo kwa lengo lililokusudiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Pilly Kitwana, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa pikipiki hiyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
"Tumepokea pikipiki 1 kutoka TAMISEMI, na kwa kuona changamoto ya umbali kwa watendaji wetu tumeikabidhi kwa Mtendaji wa Kata ya Mindu, ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi,tunaomba waitunze na kuithamini kwa kutambua kuwa ni mali ya Umma" Amesema Kitwana.
Kwa upande wa Afisa Mtendaji Kata ya Mindu, Baraka Lemaha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mgao huo wa pikipiki na kuahidi kutumia pikipiki hiyo kwa matumizi mazuri ya kiofisi ili kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuleta maendeleo.
Post a Comment