MBUNGE DKT. ABOOD, AITAKA JUMUIYA YA WAZAZI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Dkt. Abdulaziz Abood, ameitaka Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro kushirikiana kwa karibu na Jamii katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba kwa wanafunzi.
Kauli hiyo ameitoa katika Kikao cha Baraza la Wazazi Kata ya Kingolwira kilichofanyika Februari 22/2023.
Dkt. Abood, amesema ili kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto pamoja na wanafunzi wazazi Jumuiya ya Wazazi inalo jukumu kubwa la kushirikiana na Jamii kusimama kikamilifu ili kutokomeza vitendo hivyo.
" Maswala ya ukatili wa kijinsia ni jambo ambalo limeanza kwa muda mrefu ndani ya jamii zetu na ni kubwa hili pengine linaweza kuchangiwa na utandawazi, tunaona serikali imeanzisha madawati ya kijinsia mashuleni kwaajili ya watoto wa kike na hata kwetu lipo ili watoto wakike kuweza kupaza sauti kwenye haya madawati na hatimaye kupata suluhu ya matatizo yao, niombe Jumuiya ya wazazi hili mkaliundie mkakati wa kupaza sauti kwa kuwa nalo linawahusu moja kwa moja " Amesema Dkt. Abood.
Post a Comment