DC NSEMWA AWATAKA MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Rebeca Nsemwa , amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo ili kuwezesha Halmashauri kuweza kuongeza uwezo wa kujitegemea kwa mapato ya ndani ya Halmashauri.
DC Nsemwa, ameyasema hayo Februari 08/2023 katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu Manispaa ya Morogoro.
Aidha,a mesema kuwa Halmashauri ikiboresha mapato itasaidia kutoa huduma za jamii kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, Maji pamoja na kuongeza viwango vya mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.
Hata hivyo, amewataka Waheshimiwa Madiwani kutenga muda wa kupitia vyanzo vyote vya mapato ili kuweka usimamizi mzuri ambao utapelekea ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
Pia, amesema kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani lazima uendane na nidhamu ya matumizi ya fedha kwa hiyo ni jukumu la Baraza la Madiwani kusimamia na kuhakikisha kuwa mapato yote yanayokusanywa katika vyanzo vya ndani yanatumika ipasavyo.
“Niombe sana Waheshimiwa Madiwani na Watumishi hakikisheni fedha zinazokusanywa kupitia katika miradi yote zisitumike zikiwa mbichi, bali zinatakiwa kupelekewa benki na kutumika kwa kufuata utaratibu mzuri na ulio sahihi kisheria , “ Amesema DC Nsemwa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, amewataka madiwani hao kuwa na umoja na mshikamano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowasilishwa kwao kutoka kwa wananchi ili kuweza kuzitatua na kuzijadili kwa pamoja.
Fikiri , amewataka madiwani wa kata zote kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta Maendeleo katika kwa kushirikiana vyema na Uongozi wa Manispaa.
Post a Comment