MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA
MADIWANI wa Manispaa ya Morogoro, wamefanya mkutano wa kuwasilisha taarifa za kata za ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani utakaofanyika tarehe 8/2/2023.
Mkutano huo wa kuwasilisha taarifa , umefanyika Februari 6/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa.
Mkutano huo umehudhuriwa na madiwani wa kata zote 29 pamoja na Watendaji wa Kata , Wakuu wa Divisheni na vitengo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Madiwani hao waliweza kuwasilisha taarifa hizo wakiwa wameeleza mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika nyanja za elimu, kilimo, ufugaji, utekelezaji wa miradi ya maendeleo , utunzaji wa mazingira ,kiuchumi na afya.
Hata hivyo baadhi ya changamoto zilizo bainishwa ni pamoja uhaba wa maji , miundombinu ya barabara, ukosefu wa vyoo katika baadhi ya shule n.k.
Katika Kikao hicho kiliendeshwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro ambaye ni Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Mohamed Lukwale, pamoja na Katibu wa kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Jeremia Lubeleje,ambapo taarifa zote zilizowasilishwa zilipokelewa.
Post a Comment