Header Ads

KIPIRA ATEMA CHECHE KONGAMANO LA MJADALA WA FAMILIA.



MWENYEKITI wa  Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Kipira, ametoa rai kwa wazazi kujikita katika jukumu la kutoa elimu kwa jamii kuhusu suala la maadili kutokana na hivi sasa kuanza kujitokeza mfululizo wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.

Akizungumza na mamia ya waliojitokeza katika Kongamano la mjadala wa familia lililoandaliwa na Shirika la WICOF , lililofanyika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro Februari 25/2023.

Kipira,  amesema suala la malezi ya watoto ni jukumu la watu wote  kwani hivi sasa kumeanza kujitokeza mwenendo usiofaa kwa jamii katika nchi yetu.

"Kila tukikaa ndani ya siku mbili ukisikiliza vyombo vya habari wanakwambia kuna unyanyasaji wa kijinsia, mara utasikia baba kamuua mama,mara mama kauawa na mtoto au mama kaua mtoto au baba kampiga mama kipigo kikubwa,yote haya ni ukiukwaji wa maadili ambapo sasa Jamii tunahaki ya kuyakemea kwa nguvu kubwa" Amesema Kipira.

Aidha, Kipira, amesema kupitia Kongamano hilo, atashirikiana na Kamati yake ya utekelezaji kuona namna gani ya kuandaa Kongamano kama hilo ili kufikisha elimu zaidi kwa wananchi.

Mwisho, amelipongeza Shirika la WICOF kwa kuandaa mjadala wenye kulenga kupunguzana kuondoa kabisa vitendo vya kijinsia lakini kuelimisha jamii juu ya malezi ya watoto.

Naye, Mkurugenzi wa WICOF , Mwajabu Dhahabu, ameipongeza Jumuiya ya Wazazi kwa namna inavyoshughulikia changamoto za Malezi.

"Tuwapongeze ndugu zetu wa Chama, suala la malezi ni letu sote, naamini kila mmoja akismama kwa nafasi yake , hizi changamoto zinazojitokeza katika malezi zitapungua au kumalizika kabisa" Amesema Mwajabu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.