Header Ads

KIPIRA AWATAKA JUMUIYA YA WAZAZI KUDUMISHA UPENDO


WANACHAMA wa Jumuiya ya Wazazi  CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, wametakiwa kutotengeneza Maadui badala yake  kuishi vizuri kwa ushirikiano ili kuwaonyesha CCM iliyo imara.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, CDE. Salum Kipira katika ufunguzi wa Baraza la Wazazi Kata ya Kihonda Maghorofani Februari 22/2023 katika Ukumbi wa Idiva.
"Jumuiya yetu ni moja, hata katika timu yangu ya Kamati ya utekelezaji tunaishi vizuri, niwaombe wana Jumuiya Wilaya ya Morogoro Mjini tujihadhari na Maadui wa nje na ndani ambao wanataka kutufanya tugombane ili waweze kuuza silaha kwa kuwa wamoja na kujenga mashikamano ndani yetu" Amesema Kipira.
Aliwaonya wanajumuiya ambao wana nia ya kugombea 2027  kutofanya kampeni mapema na kusubiria muda utakapofika kwani Jumuiya na chama vinautaratibu wake uliojiwekea katika kipindi cha uchaguzi unapofikia.
" Tumemaliza uchaguzi salama, tufanye kazi ya kumsaidia Rais wetu na Chama chetu, sio muda wa majungu na kunyoosheana vidole tufanye kazi ,wananchama walituamini na sisi tuwaonesha imani kwao, yapo mambo Serikali inafanya makubwa, hayo sisi ndio ya kuyasemea na sio kutengenezeana chuki ambazo hazina afya ndani ya Jumuiya yetu" Ameongeza Kipira.

Amesema kuwa kwa Sasa jumuiya ipo katika hatua nzuri ya kuacha utegemezi na ombaomba kwani tayari inaendelea na miradi midogo na mikubwa kama mradi wa tisheti na mradi wa Samaki ambapo Kamati ya Uchumi na fedha inaendelea na uratibu nwa miradi hiyo.
Kwa upande wake, Katibu Malezi Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Godwin Mlambiti, amewataka Makatibu Malezi kuhakikisha wanafanya ziara za mashule ili kujua changamoto zinazowakumba wanafunzi na kuanza kampeni za kupinga ukatili wa kijinsia.
Mlambiti amesema Jukumu la Malezi ni kuhakikisha wanafunzi shuleni wanapata malezi mazuri na kuwa na mafunzo ambayo yatawafanya wanafunzi kuepukana na changamoto za Ulawiti, ubakwaji.
Naye Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Eng. Hamisi Ndwata, ameipongeza Jumuiya ya Wazazi kwa kazi inazozifanya za kuimarisha uhai wa chama.
Ndwata, amesema kwa sasa Kihonda Maghorofani ipo shwari kwani changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi, changamoto ya huduma ya afya,  madawati pamoja na msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Kihonda Maghorani vyote ameanza kuvitatua ambapo changamoto ya miundombinu ndio ambayo imekuwa ikmuumiza kichwa.
Mwenyekiti wa Wazazi Kihonda Maghorofani, Ndg. Boma Kibaja, amesema kuwa Jumuiya upande wa Kata yake imejipanga vizuri kuhakikisha inafanya ziara shuleni pamoja na kuweka mikakati thabiti ya kutatua kero na kukisemea chama cha Mapinduzi  na Serikali yake.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.