UWT WILAYA YA MOROGORO MJINI YAADHIMISHA MIAKA 46 YA CCM KWA KUGAWA MASHUKA KITUO CHA AFYA MAFIGA NA UPANDAJI WA MITI
KATIKA kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, UWT Wilaya ya Morogoro Mjini imeadhimisha maadhimisho hayo kwa kugawa shuka wodi ya wakina mama pamoja na vinywani , sabuni pamoja zoezi la usafi na upandaji wa miti.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Januari 29/2023, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini, Victoria Saduka, amesema maadhimisho hayo yatakuwa endelevu kwa miaka yote ya kuwakimbilia watu wenye uhitaji.
"Kituo hiki cha afya kinazidi kukuwa, kila uchwao idadi ya wagonjwa wanaongezeka, hivyo katika kuona wapi tunakwenda kupeleka baraka zetu, tumeona tufike hapa tugawe kila ambacho tumejaliwa, sisi kama wakina mama tunafahamu uchungu wa wenzetu hawa waliopo hapa Kituo cha afya , tutaendelea kushirikiana lengo ni kutekeleza Ilani ya CCM katika upande wa Sekta ya afya " Amesema Saduka.
Saduka, amesema Serikali kwa kutekeleza Ilani ya CCM itaendelea kutoa fedha kwa ajili kuboresha huduma ya Afya kwa jamii.
"Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM na sisi tumejionea utekelezaji mzuri wa ilani yetu, tukasema kama Wanawake wa Wilaya ya Morogoro Mjini hebu tuje pia kuweka mchango wetu wa mashuka hapa Kituo cha Afya cha Mafiga ," Ameongeza Saduka .
Naye, Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini,Aziza Hussein, amesema juhudi kubwa za kimaendeleo zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndizo ambazo zimewafanya waone kwamba nao wanapaswa kumuunga mkono kwa kuchangia vifaa hivyo.
" Tumeguswa sana na kazi kubwa anayofanya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amejenga vituo vingi vya afya nchi nzima, sisi Manispaa ya Morogoro tuna vituo vya afya vikubwa tena vyenye hadhi ya Hospitali kabisa, haya mashuka tuliyoleta hapa Mafiga ni kuonesha jinsi gani tunamuunga mkono" Amesema Aziza.
Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mafiga, Dr. Anjelista Bigumile, ameushukuru Uongozi wa UWT Wilaya ya Morogoro Mjini kwa kwa msaada huo kwani utawasaidia kwa kiasi kikubwa wahitaji.
Post a Comment