Header Ads

NAIBU WAZIRI AWAHAKIKISHIA WATANZANIA KUWA MAWASILIANO NAO NI KIPAUMBELE CHA SERIKALI HIVYO ITAIMARISHWA.


NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ICT) - Mhe. Mhandisi. Andrea Mathew Kundo amemwagiza Mkuu wa Kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA), Kanda ya Mashariki kushughulikia haraka maombi ya Halmashauri ya Chalinze ya kuimarisha MIundombinu ya mawasiliano ikiwemo kupatiwa kibali cha  Masafa ya radio (radio frequency) na Televisheni ambayo yalikwama kwa muda.

Pia Halmashauri imepokea vifaa kwa ajili ya kupimia Ardhi. Vifaa hivi vinasaidia kurahisisha Upimaji. Vifaa hivi vitawezesha kwa siku kupimwa kwa viwanja hadi 200 toka utaratibu wa kawaida wa viwanja 5.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.