Header Ads

DC MSULWA AWAASA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MANISPAA YA MOROGORO WAASWA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA.

 

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (wapili kutoka kulia) akiongozana na ,   Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro , Mhandisi Joyce Baravuga (wa kwanza kutoka kulia ), Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba (watatu kutoka kulia) wakati wa kukagua  mabanda ya maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (wa tatu kutoka kushoto ), akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (katikati) Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba na Madiwani wa Manispaa ya Morogoro  wakati wa kukagua  mabanda ya maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali.

Mwenyekiti wa CCM Morogoro Mjini , Ndg. Fikiri Juma  (kulia ) , Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (kushoto ), Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro , Mhandisi Joyce Baravuga (katikati  )wakikagua mitungi ya fire katika banda lao la maonesho.






MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewaasa wajasiriamali Wanawake Manispaa ya Morogoro  kuzingatia umuhimu wa ubora kwenye bidhaa zao wanazozalisha kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ili kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo ameitoa Machi 08/2021 katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Manispaa ya Morogoro yaliyofanyika katika Ukumbi wa Morena Msamvu.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Msulwa, amesema kuwa ufungashaji bora wa bidhaa  pamoja na uwekaji wa nembo na sehemu bidhaa zinapozalishwa na kutokea  ndiyo njia pekee itakayowakomboa wajasiriamali ili kuingia kwenye soko la ushindani.

"Nimetembelea katika mabanda yote, nimefurahishwa sana na ubunifu wa bidhaa, lakini kuna vitu viwili vinakosekana ikiwamo kutoonesha bidhaa hiyo inatoka wapi hilo ni kosa moja la kiufundi , lakini jambo jengine ni viwango vya mashakamashaka, maana ya viwango tafuta  kakopo kazuri weka namba zako za simu  ambazo zitawasaidia wateja kukupata maana ukichukua kitu harafu hakijulikani kimetoa wapi ni tatizo , Morogoro Vijijini wazalishaji wazuri wa karafuu, hapa nimeona karafuu, iriki, mdarasini  , vanila, vyote hivyo ni fedha hivyo  katika bidhaa zetu tutengeneze zikiwa zinazingatia ubora ili kuweza kupata soko la uhakika nje na ndani, lakini niwaombe sana wakina Wananchi wa Manispaa ya Morogoro mjenge utamaduni wa kununua   bidhaa zinazotengenezwa na waza , tukifanya hivyo tutakuwa tunawanyanyua wazawa na kuweza kutengeneza fursa nzuri za kutangaza bidhaa zetu na kutengeneza masoko makubwa" Amesema DC Msulwa.

Mwisho, ametoa wito kwa maafisa biashara na Uongozi kwa ujumla kuweza kuwainua  wafanyabiashara wadogowadogo wanaozalisha bidhaa ili kuwaelekeza ni kwa  jinsi gani kuwaongeza  thamani katika bidhaa wanazozalisha ili mwisho wa siku waweze kupata malipo stahiki yanayo wahusu.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.