Header Ads

KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI MANISPAA YA MOROGORO YAPONGEZA JITIHADA ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Kamati ya fedha na uongozi, Mhe. Pascal Kihanga (katikati),akizungumza jambo na mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni   Diwani wa Kata ya Mwembesongo ,Mhe. Ally Kalungwana wakati wa ziara kukagua miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Kamati ya fedha na uongozi, Mhe. Pascal Kihanga (kushoto), akipokea taarifa ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Ghorofa iliyopo Kata ya Boma.


Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwale, akiwa na mjumbe wa Kamati ambaye pia ni Afisa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Pendo Chagu.

Madarasa mapya ya shule ya Msingi Ujirani Kata ya Mkundi.

Mjumbe wa Kamati ya fedha na Uongozi na Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe.Ally Kalungwana, akichangia maada katika majumuisho ya kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi Ukumbi wa Kilimo Manispaa ya Morogoro.

KAMATI ya Fedha na Utawala  Manispaa ya Morogoro  imeridhishwa na kupongeza hatua ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku ikisisitiza miradi ambayo haijamalizka ikamilike kwa wakati ili iendelee kuwanufaisha Wananchi.

Hayo yamejiri Machi 17/2021  wakati ikifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa   katika kipindi cha   mwaka wa fedha 2019/2020.

Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu , Mhe. Pascal kihanga,  walijionea hatua za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Ujirani iliyopo Kata ya Mkundi, Ujenzi wa  shule mpya ya Sekondari iliyopo Kata ya Mkundi yenye vyumba 6 ambavyo kati madarasa hayo, vyumba 3 vimejengwa kwa nguvu ya Wananchi na vyumba 3 kupitia fedha za Diwani wa Kata ya Mkundi Mhe. Seif Chomoka.

Aidha, kamati hiyo , mbali na kutembelea miradi ya shule lakini walitembelea mradi wa Jengo la Wanawake Wajasiriamali Wasindikaji wa vyakula mbalimbali lililopo Kata ya Kihonda Maghofani, Maabara Kituo cha afya cha Mafiga, Ujenzi wa shule mpya ya Ghorofa ya Sekondari Kata ya Boma pamoja na kutembelea jengo la kitega uchumi DDC .

Kamati hiyo, imesema kukamilika  kwa miundombinu ya shule  kutasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na hivyo kutekeleza kwa ufanisi sera ya elimu bila malipo.

Pia imesema katika miradi hiyo ipo miradi ambayo itapelekea kuchangia ongezeko la pato la ndani ikiwemo mradi wa kitega uchumi wa DDC .


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.