Header Ads

RC SANARE AWATAKA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUSIMAMIA UJENZI WA MADARASA NA KUPIGA VITA MIMBA ZA UTOTONI.












Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kusimamia na kuhimiza ujenzi wa vyumba vya madarasa na samani zake,kupiga vita mimba za utotoni.

Kauli hiyo ameitoa leo Machi 04/2021 katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Morogoro kinachofanyika Ukumbi wa  Chuo Cha ualimu Kigurunyembe Manispaa Morogoro.

 Pia amewataka Wakurugenzi  kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na kukamilisha usajili wa majengo na mabango kwa ajili ya kutozwa kodi ya majengo ma ushuru wa mabango.

Katika hatua nyengine, amewaagiza   wa Wakuu wa Wilaya  kusimamia agizo la serikali la kuendeleza kilimo cha mkonge.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.