Header Ads

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA YA MIKOPO KUJIENDELEZA KIUCHUMI


Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ,  Sheilla Lukuba, (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya bidhaa inayozalishwa na wanufaika wa mkopo kutoka kikundi cha Kasi Mpya na Silk kilichopo Kata ya Kihonda.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, akiwa pamoja na Wakuu wa Idara na viongozi wa Kikundi cha ujasiriamali cha Kasi Mpya na Silk katika picha ya pamoja .
Mmoja wa kiongozi kutoka Kampuni ya uzoaji wa Taka ya M2 Smart akisoma taarifa ya kampuni yao mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro akitoka kufanya ukaguzi katika Ofisi ya M2 Smart Kampuni ya Taka .
Baadhi ya Wakuu wa idara wakionekana kufurahishwa jambo mara baada ya mazungumzo kuamalizika wakati wa ziara ya kutembelea Kampuni ya usafi ya M2 Smart.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, akikagua duka la Kikundi cha  watu wenye ulemavu kilichonufaika na mkopo wa asilimia 10 wa Manispaa  kilichopo ndani ya  Stendi ya mabasi Msamvu  
Mmoja wa wanakikundi cha watu wenye ulemavu Msamvu Stendi akiwa dukani kwake.



                                            





MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kutumia fursa ya mikopo kujiendeleza kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa leo Machi 12/2021 ikiwa ni siku moja kupita tangia kufanyika kwa Mkutano wa kujadili  mapendekezo ya bajeti ya fedha ya mwaka 2021/2022 akiwa katika ziara aliyoambatana na Wakuu wa Idara wa Manispaa ya Morogoro ya kukagua baadhi ya  vikundi vya vilivyokopeshwa  mikopo ya asilimia 10.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kuwa Manispaa ya Morogoro inaendelea kuwawezesha wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu  ili kuweza kujiinua kiuchumi na itawasimamia katika kuhakikisha kuwa mikopo hiyo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inawanufaisha Wananchi.

" Naahidi kuendelea kuwaendeleza wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu  kiuchumi kwa kuwashika mikono kwa kutoa mikopo ya asilimia kumi katika mapato ya ndani,  kupitia idara ya maendeleo ya jamii nitaendelea kuwainua wananchi wa Manispaa ya Morogoro , lakini niwaombe hizo fedha mnazokopeshwa ziwe katika mzunguko na zirudishwe kwa wakati ili wengine wapate" Amesema Lukuba.

Lukuba, amesema kuwa , mikopo hiyo  sio zawadi inayotolewa kwao bali wanatakiwa kurejesha kwa wakati ili kuongeza wigo wa utoaji mkopo kwa vikundi vingine vingi zaidi na kukuza uchumi wa wananchi kwa vikundi  na mtu mmoja mmoja.

Katika hatua nyengine, Lukuba, amesema kuwa kwa  mwaka huu wa fedha 2021/2022 Manispaa ya Morogoro imetenga kiasi cha zaidi ya Tshs.963,000,000.00 kwa ajili ya mkopo wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu .

Katika ziara ya leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na Wakuu wa idara wametembelea madarasa 4 yaliyojengwa na TASAF   kwa kila shule  kwa shule mbili za Sekondari ikiwamo Shule ya Sekondari SUA na Mafiga pamoja na kuangalia ujenzi wa Shule Sekondari SUA .

Lakini pia ukaguzi wa Kikundi kazi cha ndani kilichopata tenda ya uzoeaji wa takataka kupitia mkopo wa Manispaa cha M2 Smart , Kikundi cha ujasiriamali wa kushona Masweta cha Kasi Mpya na Silc Kata ya Kihonda, Duka la huduma za kifedha na bidhaa za vyakula la  watu wenye ulemavu  lililopo Stendi ya Mabasi Msavu ikiwa na lengo la kuona maendeleo ya vikundi hivyo na kuona kama fedha walizopewa zimetumika kwa malebngo yaliyotarajiwa.  

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.