BARAZA LA MADIWANI JIJI LA DAR ES SALAAM LA MPONGEZA MHE. RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI.
Baraza la Madiwani Jiji la Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Meya wa Jiji la Dar es salaam Wilaya ya Ilala *Mhe Omary Kumbilamoto* limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dkt John Pombe Magufuli* kwa kuipandisha hadhi Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es salaam.
Pongezi hizo zimetolewa na Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe *Omary Kumbilamoto* wakatika akifungua kikao cha Baraza Madiwani wa Jiji la kupitisha Makadilio ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kilicho fanyika katika Ukumbi wa Antoglo Dar es salaam.
Aidha *Mhe. Kumbilamoto* aliainisha baadhi ya sababu amabazo zimemfanya Mhe. Rais kuichagua Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es salaam;
" Zipo sababu ambazo zimeifanya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji 1. Manispaa ya Ilala tumepata hati safi kwa miaka 5 mfurulizo, 2. Tumeongoza kwa ukusanyaji wa Mapato Nchi nzima, 3. Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo, 4. Utoajia wa Asilimia 10 kwa Vijana, Wanawake na Walemavu hongereni sana Madiwani, Mkurugenzi pamoja na timu yako" alisema *Mhe. Kumbilamoto*
Lakini pia Mhe. Kumbilamoto ameendelea kusema watu ambao wanaobeza kwenye Mitandao ya Kijamii Zingiziwa kuwa sehemu ya Jiji na Masaki kuwa sio sehemu ya Jiji wanasahu kuwa yapo maeneo katika baadhi ya Miji yana unafuu kushinda Zingiziwa;
" Ukienda Kenya katika Mji wa Nairobi kuna sehemu inaitwa Kibera huwezi kuifanisha na Zingiziwa lakini ipo kwenye Mji wa Nairobi hivyo hivyo ukienda Namibia katika Mji wa Windhoek kuna sehemu inaitwa Katutura huwezi pia kufanisha na Zingiziwa ila ipo katika Mji hivyo Zingiziwa kuwa sehemu ya Jiji imestahili" Alisema *Mhe. Kumbilamoto*
Baraza hilo limeweza kupitisha Mpango na Bajeti wa mwaka 2021/2022 unajumla ya Tshs *218,004,242,381/=* kati ya fedha hizo Tshs *62,000,000,000/=* ni fedha kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri na Tshs *156,004,242,381/=* ni fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu ambapo kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na Matumizi ya kawaida.
Katika Bajeti ya mwaka 2021/2022 Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii inatarajia kutumia jumla ya Tshs. *20,783,941,240/=* kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, ambapo Tshs. *14,158,883,999/=* ni fedha kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri na Tshs. *6,625,057,241/=* ni fedha kutoka Ruzuku mbalimbali.
Fedha zitakazotumika kwa ajili ya Matumizi mengineyo ni jumla ya Tshs. *4,747,247,000/=* ambapo Tshs. *2,233,000,000/=* ni fedha kutoka Ruzuku mbalimbali.
Miradi itakayotekelezwa na Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii katika mwaka 2021/2022 ni pamoja na;-
1. Sekta ya Elimu Msingi
2. Sekta ya Elimu Sekondari
3. Sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii
4. Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Ukimwi na Vijana
5. Sekta ya Mifugo na Uvuvi
6. Sekta ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
7. Kitengo cha Nyuki.
Post a Comment