TAASISI YA NGAIZA FOUNDATION YASIMAMA BEGA KWA BEGA NA MHE.RAIS SAMIA, YASEMA INA IMANI KUBWA NA UONGOZI WAKE.
Shirika la kutetea haki za Wanawake na Watoto wa kike la Ngaiza Foundation limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais na kueleza kuwa wana matumaini makubwa na uongozi wake na Wanaamini ataifikisha Tanzania mahala panapostahili.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Elizabeth Ngaiza amesema Mhe. Samia ameudhihirishia ulimwengu Kuwa Mwanamke Mwanamke akipewa nafasi anaweza kufanya Mambo makubwa na kitendo Cha kuwa Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania kimezidi kuwapa Hari na matumaini makubwa Wanawake.
Ngaiza amesema kwa Sasa ni wakati muafaka kwa Wananchi kumpa ushirikiano wa kutosha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kutimiza maono makubwa aliyonayo kwa Taifa la Tanzania.
Aidha Ngaiza ameeleza kuwa Taasisi yake imekuwa na Imani kubwa na Mhe. Rais Samia tokea alipoonyesha uwezo mkubwa wakati wa Bunge la Katiba adi nafasi ya Makamu wa Rais hivyo hawana mashaka yoyote na utendajikazi wake sababu tayari alishaonyesha uwezo Mkubwa kwenye kila nafasi aliyoshikilia.
Pamoja na hayo amebainisha kuwa lengo la kuanzisha Shirika la Ngaiza Foundation ni kutoa jukwaa la wanawake na Watoto wa kike kupaza sauti zao na kutetea haki zao na tangu kuanzishwa kwa shirika hilo imesaidia wanawake wengi kupata haki na Elimu juu ya haki.
Itakumbukwa kuwa Tanzania ni moja ya nchi zilizoridhia mikataba na matamko mbalimbali ya Kimataifa yanayotoa haki kwa kila mtu kushiriki katika utawala wa nchi, haki za kisiasa na kiraia na mingine inayotoa miongozo ya ushiriki sawa wa kijinsia.
Post a Comment