ABOOD ATOA HUNDI YA MILIONI MOJA JUKWAA LA WANAWAKE MAZIMBU, HUKU AKIWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA MIKOPO YA SERIKALI ISIYO NA RIBA.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, (kulia) akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Mazimbu, Bahati Mwale.
Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 1 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abood.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, akimkabidhi mmoja wa wananchi vyakula.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, akimkabidhi jezi pamoja na mpira kiongozi wa timu ya mpira wa miguu ya Spider FC iliyopo Kata ya Mazimbu.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, akikabidhiwa cheti cha shukrani na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Mazimbu, Bahati Mwale.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Mazimbu na Kamati ya maandalizi kwa Mhe. Abood kwa kukubali wito wa Kata hiyo kuhudhuria maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Kiongozi wa timu ya mpira wa miguu ya Spider akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa mpira na jezi na Mhe. Abood.
Mtendaji wa Kata ya Mazimbu, Prisca Mawala, akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kata ya Mazimbu.
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Kata ya Mazimbu wakiwa katika furaha ya aina yake katika maandalizi ya siku ya Wanawake Duniani Kata ya Mazimbu.
Kamati ya maandalizi wakiwa pamoja na Uongozi.
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, ametoa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni moja (1,000,000/= ) kwa Jukwaa la Wanawake Kata ya Mazimbu huku akiwataka Wanawake wa Jimbo hilo pamoja na Kata zote Manispaa ya Morogoro kuchangamkia mikopo ya Serikali isiyo na riba.
Abood, ameyasema hayo hayo Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro leo Machi 06/2021 wakati wa akizungumza na Wanawake wa Kata hiyo katika sherehe za maandalizi ya kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Manispaa ya Morogoro.
Abood, amewataka Wanawake wa Jimbo la Morogoro Mjini kukopa pesa hizo na kuzitumia kwa malengo yaliokusudiwa sambamba na kupeleka marejesho ya mikopo ili wengine waweze kukopa.
"Serikali umetenga imetenga fedha za mikopo isiyo na riba katika jimbo langu wamama,vijana changamkieni mikopo hiyo ili muweze kukuza mitaji yenu, nimeguswa sana na Wakina mama nimeona nitoe Shilingi Milioni moja kwa Jukwaa la Wanawake wa Mazimbu, niwaombe hizi fehda mzitumie vizuri watu wakope na kurudisha ili wengine waweze kupata fedha hizi ziwe katika mzunguko lengo likiwa ni kuwakomboa wakina mama wote waliojiunga katika Vikundi ili kujikwamua kiuchumi " Amesema Abood.Aidha kwa upande mwingine , Abood, amesema yeye ndio Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini , ndio atatatua changamoto za Wananchi kwa sasa yupo Jimboni kwa ajili ya kushughulikia kero zote.
Amesema kuwa , anatarajia kuandaa mkutano Mkubwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wake hivyo wasikate tamaa,miradi yote itatekekezwa kwa fedha za Serikali .
Wakati huohuo Abood, amesema ni kuweza kukutana na Vikundi vya wajasiriamali katika kuvijengea uwezo.
Kihanga, amewataka wanawake kujikwamua kiuchumi katika kujishughulisha na biashara na kukuza mitaji yao kuacha maisha tegemezi .
Pia amewataka wanawake kuchangamkia fursa za biashara na kutangaza bidhaa zao katika masoko mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Mazimbu, Bahati Mwale, amesema kuwa dhumuni kuu la Jukwa la Wanawake ni kuhakikisha Wanawake wote wa Manispaa wanaingia katika mpango maalumu wa vikundi ili waweze kukopesheka na kunufaika na mkopo wa Manispaa wa asilimia 10 usio na riba.
Post a Comment