RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Mashishanga ,ametoa salamu za pole kwa watanzania wote kwa jumla kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyefariki Dunia Machi 17 Machi, 2021.
SalamU hizo amezitoa Machi 19, 2021 alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo.
Katika salam zake mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, ametoa rai kwa viongozi wa Serikali kumpa ushirikiano Rais wa awamu ya sita ayeapishwa leo Mhe. Samia Suluhu Hassan ili kuendeleza yale mazuri ambayo Dkt. John Pombe Magufuli ameyaacha.
Aidha, amewataka watanzania kumuenzi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchapa kazi ili kuinua uchumi wa nchi hiii, kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu na kumtanguliza mungu katika kazi zote watakazokuwa wanazifanya
Post a Comment