Header Ads

Wasanii Watakiwa Kutengeneza Kazi nzuri zitakazovutia Wadhamini.

            

              

                

Serikali imewataka wasanii kutengeneza kazi nzuri zenye ubora zinazozingatia maadili ya Kitanzania ili kuwavutia wawekezaji wengi wanaotaka kudhamini kazi hizo katika kuziandaa na kuzisambaza.


Hayo yamesemwa leo Machi 06/2021 Manispaa ya Morogoro na Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo, wakati akizungumza na Wasanii Manispaa ya Morogoro katika Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu.

“Nimefurahishwa sana na mwitiko wa Wasanii, huu ni mkutano wangu wa kwanza na Wasanii wa Morogoro, natumaini kabisa kwa mwitiko huu tunakwenda kubadilika na kuanza kuandaa kazi nzuri zenye viwango ili kuweza kujitengenezea Soko""Amesema Dkt. Kilonzo.


Aidha amewataka Wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ambazo zitakidhi vigezo vyinavyotakiwa.

Mwisho, amewaasa Wasanii kufanya kazi zenye viwango ambazo zitakuwa na ubora na zenye kuzingatia maadili .

Naye, Afisa Utamaduni Manispaa ya Morogor, Safia Kingwahi, amewataka Wasanii kufanya kazi zenye viwango na kuzingatia sheria na taratibu zinazoongoza tasnia ikiwamo usajili na vibali kutoka  Bodi ya Filamu .
Aidha, amewataka Wasanii kutumia Masoko yaliyopo kuengeneza kazi zenye ubora badala ya kuendelea kulalamika.

Kwa upande wa Mshauri wa Waigizaji Mkoa wa Morogoro, Haviti Makoti, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Filamu kwa kikao chake huku akiahidi kumpatia ushirikiano.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.