Header Ads

DC MSANDO AZITAKA HALMASHAURI KUWA NA MPANGO BORA WA ARDHI ILI KUEPUSHA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI.

 

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msnado, akizungumza na wananchi nyumbani kwa marehemu Godfrey Kanuti wakati wa kutoa pole kwa familia ya marehemu aliyeuwawa kwa kuchomwa mkuki kifuani .

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msnado, akisalimiana na baba mzazi wa marehemu Godfrey Kanuti nyumbani kwake Kata ya Bwakila chini.

Nyumbani kwa marehemu Godfrey Kanuti.

DC Msando, akiwa katika picha ya pamoja askari wa wanyama pori wa hifadhi ya JUKUMU.

DC Msando, akiwa jirani na zizi la ng'ombe waliokamatwa na JUKUMU .

Ng'ombe waliokamatwa na jumuiya ya JUKUMU kufuatia wenye ng'ombe hao kuwatelekeza baada ya kufanya mauaji.

DC Msando, akikagua jengo la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.


Jengo la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogor

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amezitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa zinakuwa na mipango bora ya ardhi ili kuweza kuzuia migogoro ya wakulima, wafugaji pamoja na wahifadhi.

Hayo ameyasema Juni 23/2021 wakati wa ziara yake ya kupokea taarifa juu ya kuuwawa kwa askari wa wanyama pori wa  Jumuiya ya kuhifadhi matumizi bora ya wanayama pori Bonde la UKUTU kwa vijiji 11 vilivyozungukwa na hifadhi ya Nyerere National Park (Gonabis Kidunda) WMA, Ndg. Godfrey Kanuti na kutoa mkono wa pole kwa familia ya Kanuti aliyeuwawa  kufuatia kuchomwa mkuki wa kifuani na watu wasiojulikana kutoka jamii ya wafugaji.

 Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Mvuha na Bwakila , amesema kuwa wanakijiji wanapaswa kuzisimamia Serikali zao za kijiji ili ardhi yao isichukuliwe bila kufuata utaratibu kwani kuna baadhi ya sehemu baadhi ya viongozi wamekuwa sio waaminifu wanagawa ardhi ya kijiji bila kuwashirikisha wenye ardhi yao.

“Nataka  migogoro ya wakulima, wafugaji na wahifadhi iwe historia, niseme kuwa msimamizi mkuu wa ardhi ya Kijiji ni Serikali ya kijiji kupitia mkutano mkuu, mtu yeyote anaehitaji kumiliki ardhi ya kijiji anatakiwa kupitishwa kwenye mkutano mkuu ili apangiwe matumizi ya ardhi aliyoiomba, Mtendaji na Mwenyekiti kazi yao ni kupokea maombi tu, ardhi ni kitu cha muhimu, tusipoisimamia vizuri tutakuja kupigana wenyewe kwa wenyewe na kusababisha mauaji kama haya yaliyotokea kwa mpendwa wetu Godfrey Kanuti ”Amesema DC msando.


DC Msando, amesema kuwa  kijiji kinatakiwa kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwani itaondoa migogoro ya mipaka mbalimbali vilevile ni chombo kinachoonesha ni kiasi gani cha ardhi kilichopo kwa ajili ya shughuli za kijiji kama mifugo, kilimo, makazi, viwanda pamoja na matumizi mengine.

Hata hivyo, amesema kuwa ardhi haiongezeki bali wanadamu na mifugo ndio vinaongezeka kwa kasi hivyo ni muhimu Serikali za vijiji kuweka kipaumbele mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Kufuatia malalamiko ya wanakijiji kutolipwa fedha za gawio na JUKUMU tangia mwaka 2012 pamoja na askari pori kutolipwa stahiki zao , DC Msando, ameuagiza Uongozi wa JUKUMU kulipa deni la askari pori hao la shilingi milioni 25 japo sio kwa mkupuo mmoja lakini kwa awamu ili nawao waweze kujikimu kimaisha.

Pia, ameuagiza Uongozi wa wa JUKUMU  waweze kutoa fedha ya fidia kwa marehemu isizidi ndani ya wiki mbili fedha hizo ziwe zimefika kwa familia hiyo.

"JUKUMU kwa upande mwengine imekuwa ikisaidia sana maendeleo ya Vijiji ikiwemo kuongeza kasi ya maendeleo katika Vijiji huduma ya elimu, shule, maji , umeme kwahiyo niwaagize maafisa Maliasiri hakikisheni mnatenga muda wenu kutoa elimu kwa wananchi juu ya manufaa ya JUKUMU lakini pia Viongozi wa JUKUMU nao hakikisheni mnawajulisha wananchi juu ya mkataba wa mwekezaji ikiwemo kuwasomea mapato na matumizi ili kuondoa minong'ono mitaani" Ameongeza DC Msando.

1.Pia amewaagiza  viongozi kuweza kuongeza tija katika suala zima la kilimo, ufugaji na jinsi ya kuweza kutataua kero za wananchi zinazowakabili.

laLakini pia amewataka wananchi wasihatarishe maisha ya askari wa wanyama pori kwani wanatakiwa waishi kama marafiki kwa kusaidia kufanikisha JUKUMU inasonga mbele na inawapatia maendeleo.

1. Pia amewataka viongozi wa JUKUMU kuomba radhi kwa wananchi kutokana na kutokutoa taarifa zinazoendelea katika Jumuiya hiyo jambo ambalo limekuwa likileta maswali mengi kwa jamii.

a Amewataka viongozi wa Vijiji na ngazi ya Kata kujenga utaratibu wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi ili kuweza kusogeza huduma na kuwapatia maendeleo ikiwemo  kusoma mapato na matumizi katika mikutano yao ikiwamo kubandika taarifa hizo katika maeneo mbalimbali ya wazi ili hata wale wananchi waliokosa vikao waweze kupata fursa ya kusoma taarifa hizo.



KKatika hatua nyengine,  amemuagiza kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kumpatia huduma ya bila malipo mama wa marehemu Godfrey Kanuti kufuatia marehemu huyo kuwa tegemezi wa familia na mama yake mzazi ni mgonjwa na marehemu ameacha watoto 5.

Mbali na hayo, DC Msnado, alipata muda wa kufika katika nyumba anayoishi familia ya marehemu ,Godfrey Kanuti, na kutoa pole kwa niaba ya Ofisi ya Wilaya huku akiwataka Wazazi,  ndugu, rafiki pamoja na jamaa wa marehemu kuwa na watulivu katika kipindi hiki cha mpito akisema kuwa Serikali inafuatilia kwa ukaribu sana na kuhakikisha wale wote waliofanya tukio hilo watatiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.

Hata hvyo, Mkuu wa Wilaya alipata fursa ya kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Tarafa ya Mvuha huku akitoa maagizo mbalimbaliikiwemo kuwataka wananchi kutoa dhana ya kusema wao wafugaji na sisi wakulima , na wahifadhi huku akiwataka wote kuwa kitu kimoja.

Akiendelea na ziara yake, DC Msando, ametoa pongezi kutokana na  jitihada za ujenzi zinazoendelea za Ujenzi wa Hospitali ya Halamsahauri ya Wilaya  huku akimtaka mhandisi wa Halamashauri kuhakikisha ujenzi huo unakamalika ndani ya muda ulipangwa.

Mwisho, emeendelea kuwahakikishia usalama wananchi  wanaozungukwa na hifadhi hiyo huku akaiwataka washikamane, na kudumisha umoja kwani   kama maeneo ya misitu na malisho ya mifugo yamehifadhiwa na kijiji ni vyema kila mwananchi akahusika kuyalinda maeneo hayo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.