Header Ads

TAS MKOA MOROGORO YATOA PONGEZI KWA WADAU WALIOFANIKISHA MISS INTERNATIONAL ALBINISM AWARENESS DAY 2021

Miss International Albinism Awareness Day 2021 Selina Alex Marcel.

Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Morogoro, Hassan Mikazi.

Hongera Sana ,Miss Selina Alex Marcel* kwa kushinda Taji la *Miss International Albinism Awareness Day 2021* na kuwa balozi wa kutetea haki na utu wa watu wenye ualbino nchini Tanzania na Duniani kwa Ujumla. TAS, inakuhakikishia  Kukupa ushirikiano wa hali na mali  katika kutimiza majukumu yako. 

Aidha niwapongeze washiriki wote walio shiriki kuwania Taji hili  na kufika hadi hatua ya mwisho nimatumaini yangu hamtakata tamaa kuwania mataji mengine pale fursa inapotangazwa. 

TAS  inawatambua washiriki wote ni Mabalozi wazuri wakuteta haki na utu watu wenye ualbino. Nimatumaini yangu kuwa jamii  itampa ushirikiano wakutosha Miss IAAD 2021 kutimiza majukumu yake. 

TAS itaendelea kufanya kazi na washiriki wote Kama Mabalozi Katika shughuli mbalimbali za kuelimisha jamii kuhusu ualbino popote pale  ndani na nje ya nchi yetu.

Kwakipekee niwashukuru wote kwakuwezesha kufanikisha tukio hiili muhimu kwanamna Moja au nyingine akiwemo Mwalimu (Trainer) Ephan Nelson, Chief Judge kaka Kudra Rajabu  na jopo lake lote,  Designers wote kwakujitolea kuwavalisha washiriki na huduma zingine walizo zitoa , wadhamini wa shuguli kwa michango yao ya Hali na mali, Mc wa shuguli hii Andrew the Host na  MCs walio saidiana nae, wanakamati ya Maandalizi kwa kushirikiana na TAS wakiongozwa na kaka Said (Kayoma) vyombo vyote vya habari na Wana habari wote wakiongozwa na wazamini wetu DZZM fm kwa chini ya usimamizi wa dada Neema Kangose , wasanii wote wakiongozwa na Dada Wastara chini ya Uratibu wa kaka Aziz (Babu) wafanyakazi wa TAS na viongozi wa TAS na  kwakipekee Serikali ya Mkoa wa Morogo chini ya idaya ya ustawi wa jamii akiwemo dada angu Rehema Malimi kwa kuwa Karibu nasi.

 Kwakipekee niwashukuru washabiki wote walio hudhuria tukio hili muhimu na la kihistoria duniani la kumpata Miss IAAD asie na ualbino lakini mwenye maono na dhamira ya dhati ya kupigania haki na utu watu wenye ualbino .

Ninaamini kupitia Mshindi wa Taji hili la Miss IAAD 2021 jamii itabadilisha mitazamo hasi dhidi ya ualbino na watu wenye ualbino nchini Tanzania na Duniani kote. 

Niwashukuru Sana na nimpongeze tena Miss Selina Alex Kwa kulitwaa Taji la Miss IAAD 2021 nakuwa balozi wa watu wenye ualbino kwa niaba ya  TAS Morogoro.  

Niwakaribishe wananchi, Mashirika na Taasisi Mbalimbali wanao hitaji kufadhili au kusaidia kufanikisha shughuli zote za Miss IAAD 2021 ili lengo lake la kuifikia jamii na kusaidia watu wenye ualbino liweze kutimia. 

Hassan Mikazi

Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Morogoro.

1 comment:

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.