DC MSANDO,AAPISHWA NA KUAHIDI KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amekula kiapo cha kuanza rasmi kuitumikia nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya, mara baada ya kuteuliwa na Mheshiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan.
DC Msando, amekula kiapo cha utii, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, Juni 21/2021 katika Ikulu ndogo ya Mkoa wa Morogoro , huku akiahidi kutekeleza kwa kasi, Ilani ya Chama cha Mapinduzi - CCM na kuwataka viongozi wa wilaya hiyo kwenda pamoja na kuwaonya, wasiotaka kutekeleza Ilani hiyo, kuachia ngazi mapema.
"Nimekuja Wilaya ya Morogoro kuwatumikia wananchi, kama Ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoelekeza nipo tayari kuitekeleza, kwa yoyote asiyetaka kutekeleza ilani ya CCM aondoke kabla sijaingia ofisini" Amesema DC Msando.
Mwisho, DC Msando, amesmhukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kumteua na kuahidi kuchapa kazi.
Post a Comment