Header Ads

NAIBU WAZIRI TAMISEMI DR DUGANGE AAHIDI KUFANYA UPANUZI WA MIUNDOMBINU KITUO CHA AFYA SABABA MANISPAA YA MOROGORO.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Festo Dugange (MB) (kushoto) akizungumza na Mganga mfawidhi wa Kituo cha afya cha Sabasaba, Dr. Vulfrida Kyara (kulia).(wapili kulia) Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kusirye Ukio.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Festo Dugange (MB), ameahidi kufanya upanuzi wa miundombinu ya wodi katika  Kituo cha afya cha Sabasaba kilichopo Mnaispaa ya Morogoro.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 18/2021 wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika Kituo hicho cha afya.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Dr Dugange, amesema ipo haja ya kituo hicho cha afya kuongezewa miundombinu ya wodi ili hata wananchi wakifika kupata huduma wapate sehemu za kulazwa kwani bado kituo hicho kina eneo la kutosha.

Dr Dugange, amesema  kuwa atahaikisha suala hilo analifikisha Wizrani ili kuona ni kwa namna gani anaweza kuona miundombinu hiyo inakamilika hata kwa kaunza kwa ujenzi wa awamu kwa awamu lengo ni kupata wodi ya kulazwa wagonjwa.

Katika hatua nyengine, Dr Dugange, ameupongeza Uongozi wa Kituo cha afya chini ya Mganga mfawidhi wa kituo hicho kwa kufanya vizuri katika eneo la makusanyo ya fedha kupitia mifuko ya afya ikiwemoNHIF ,  CHIF, pamoja na uuzaji wa dawa na huduma nyengine.

"Naamini kabisa mnanafasi kubwa ya kuendelea kukusanya fedha zaidi ya hizi mnazo kusanya kwa sasa kama mkijipanga vizuri, kwa sababu nyinyi kwa wastani kwa mwezi mnakusanya milioni 12 sawa na ukusanyaji wa shilingi 400,000/= kwa siku, kwahiyo ukijumlisha fedha za NHIF  milioni 4, CHIF milioni 2 na zile milioni 12 ambazo hazihusiani na mifuko hii ya afya mtajikuta mnakusanya milioni 18 kwa mwezi hivyo mnauwezo wa kuboresha mifumo zaidi mkapata kwa mwezi zaidi ya milioni 25 kama mkijipanga vizuri " Amesema Dr Dugange.

Aidha, Dr Dugange, ameupata Uongozi huo kwa kushirikiana na Manispaa wakae chini waweke mipango mizuri ambayo kwa sasa ni agenda ya kongeza mapato mara mbili ya hapo yanayokusanywa katika Vituo husika .

Amesema kuwa Serikali kwa sasa imedhamiria kuboresha huduma za afya ili vituo vya afya viweze kuongeza wateja wengi zaidi , wateja wasikae muda mrefu kusubiria huduma 

Hata hivyo, ameupongeza Uongozi wa Kituo hicho cha afya kwa kuwa na dawa za kutosha na mpangilio mzuri wa bohari ya dawa jambo ambalo linaonesha dalili nzuri ya kupata huduma bora na kuongeza wateja wengi zaidi.

Dr Dugange, ameutaka Uongozi wa Kituo hicho cha afya kuhakikisha kwamba wanashughulikia haraka sana changamoto za vifaa tiba ili vizweze kutumika katika kutoa huduma kwa wateja.

Amesema kuwa kuwepo kwa changamoto za vifaa tiba kunapotezea mapato kutokana na kuwakosa wateja wanaohitaji hudma za vipimo lakini kuna athiri upatikanaji wa huduma kwa wananchi .

Mwisho amemuagiza Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha afya kuhakikisha wanawahudumia haraka Wazee ili kuendana  na dahana ya Serikali ya kuanzisha dawati la kuwahudumia wazee kuliko kuwaacha wazee wakikaa muda mrefu kusubiria huduma.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.