Mdhamini wa mashindano ya CHOMOKA CUP 2021 na Diwani wa Kata ya Mkundi, Mhe. Seif Chomoka (kulia) akikabidhi vifaa vya michezo jezi na mpira kwa moja ya timu zitakazo shiriki katika mashindano hayo.
Mdhamini wa mashindano ya CHOMOKA CUP 2021 na Diwani wa Kata ya Mkundi, Mhe. Seif Chomoka , akizungumzia mashindano hayo.
MASHINDANO ya kombe la CHOMOKA CUP 2021 kuanza kutimu vumbi rasmi siku ya Julai 03/2021 katika Uwanja wa mpira wa miguu Mkundi.
Kauli hiyo imetolewa Juni 26/20221 wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya jezi na mipira kwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo na mdhamini wa mashindano hayo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro, Mhe. Seif Zahoro Chomoka.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhe. Chomoka ,amesema kuwa ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yatakuwa na vijana waliosheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa.
"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" Amesema Chomoka.
Chomoka, amewataka, washiriki wa mashindano hayo kujituma kwa bidii pamoja na kuzingatia sheria, kanuni pamoja na kuwa na nidhamu kwani mashindano hayo ni kama mashindano mengine yanayofanyika.
Aidha, amesema huo ni mwanzo lakini mashindano hayo yatafanyika kila mwaka yakiwa na lengo la kuendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wa miguu.
Amesema kuwa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ataibuka na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1 na mshindi wa pilia laki. 5.
Amesema kuwa jumla ya timu 13 zitashiriki mashindano hayo ambapo timu 10 kutoka katika Kata ya Mkundi na Mitaa yote 10 na timu mbili moja ikitokea Chuo cha Uandishi wa habari, MSJ pamoja na Chuo cha St. Joseph ambapo vyuo vyote vikimilikiwa na Diwani huyo.
Post a Comment