Header Ads

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO SHEILLA LUKUBA,ATOA VYAKULA KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

                         

Afisa Ustawi Manispaa ya Morogoro, Sidna Mathias (watatu kutoka kulia) akimkabidhi mtoto ndoo ya mafuta ya kula, ( kulia ) judith Mbelwa na (wa tatu  kushoto aliyesimama ) Rehema Malimi wote maafisa Ustawi.

                      

                       

                   

                      

MKURUGENZ wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba,amegawa vyakulà vyenye  thamani ya shilingi 200000/= kwa makao ya kulelea Watoto yatima ya The Mission To The Homeless Centre katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Morogoro .

Zawadi hiyo ya vyakula imewasilishwa na Afisa Ustawi  Manispaa ya Morogoro, Sidna Mathias, pamoja na timu yake ya Ustawi leo Juni 14/2021.

Akizungumza mara baada ya kutoa vyakula hivyo, Sidna, amesema zawadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kama ilivyokuwa kawaida yake na utamaduni aliojijengea wa kusaidia makao ya kulelea watoto.

Sidna amesema kuwa lengo la vyakula hivyo ni kuweza kuwafariji watoto ili waweze kujikuta nawao wapo kama familia nyengine.

Amesema kuwa , kama watoto watapatiwa vyakula na kuwa katika malazi mazuri basi wataishi katika misingi mizuri na kujiona wao ni moja ya watu muhimu katika jamii na kuishi kama watoto wengine wenye famil;ia zao.

"Mkurugenzi wetu amekuwa na utamaduni wa kusaidia sana makao ya kulelea watoto, kila ifikapotukio linlohusu watoto au katika sikukuu amekuwa mstar wa mbele sana kujitolea kwa gharama zake mwenye kuhakikisha anarejesha furaha kwa watoto na hata makao ya wazee pia, kiukweli amekuwa nguzo muhimu kwetu na kuona ni jinsi gani jamii inavyotakiwa kuishi na watoto yatima ili wajisikie faraja kama wanavyoishi watu wengine wenye wazazi wao" Amesema Sidna.

Miongoni mwa vyakula vilivyotolewa na Mkurugenzi ni pamoja na Unga kilo 50, sabuni ya unga kilo 15, sukari kilo 25 , mafuta ya kula lita 10 , maharage kg 15 ambapo vitu voye hivyo vina thamani ya shilingi laki mbili.


2 comments:

  1. Hongera sana kwake, Mwenyezi Mungu aendelee kumtunza mama huyu. Hakika amefanyika kua nataka kwa watoto

    ReplyDelete

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.