Header Ads

MBUNGE CHALINZE MHE. RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI BAJAJI NA TOYO KWA KIKUNDI CHA WAZALENDO.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete Akimvisha Kofia Ngumu

deleva wa Toyo wa kikundi cha WAZALENDO  ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi

vifaa hivyo kwaajili ya kuanza Kutumika.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze akitoa maelezo kuhusiana na Mradi 

mkakati ambao kupitia 10% ya mapato ya ndani Halmashauri imewawezesha vijana wa 

kikundi cha Wazalendo mbele ya Mbunge,Madiwani na Wageni waarikwa kwenye Hafla

 hiyo.


Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete (Aliesimama Mkono wa Kulia)

na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Ismail Msumi wakikata utepe kwa pamoja 

katika uzinduzi wa Hafla ya makabidhiano ya Mradi wa usafirishaji kati ya Kikundi cha 

Wazalendo na Uongozi wa Halmashauri.


Hayo yamejili juni 11/2021 katika viwanja vya Halmashauri  kwenye hafla fupi ya Makabidhiano ya vifaahivyo vya usafirishaji kati ya Uongozi wa Halmashauri na Kikundi cha Wazalendo kutoka kata ya Msata, Mbunge huyo alikabidhi Pikipiki, Bajaji na TOYO ya kubebea mizigo zenye  dhamani ya Tsh 48,384,500/= ikiwa ni sehemu ya marejesho ya asilimia kumi(10%) kwa makundi ya vijana, kinamama na walemavu kutoka katika makusanyo ya mapato ya ndani.

Akito neno la utangulizi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu Ramadhani Possi alisema, Kwa sasa Halmashauri imeamua kujikita katika kusaidia Makundi haya maalumu ili kuyainua Zaidi kiuchumi,

Tumeona tujikite Zaidi katika uwezeshaji wa Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia uanzishaji wa Miradi Mkakati, Kwa Mwaka huu tumefanikiwa kuviwezesha vikundi vinavyojihusisha na Usindikaji wa Matunda, Utengenezaji wa Samani za Mbao, ufugaji wa kuku wa kisasa na Usafirishaji kutoka kata ya Miono, Msata, Kiwangwa, Bwilingu na Pera. Alisema Ndugu Ramadhani Possi 

Hatujafanikiwa sana kwa kundi la watu wenye ulemavu kutokana na sharia iliokuwepo ilitaka wajikusanye kundi la watu wasiopungua watano ndio wapewe mkopo ila tunaamini kwa mwaka ujao wa fedha tutafanya vizuri kwani sharia hiyo imerekebishwa na inamruhusu hata Mtu mmoja kukopa katika kundi hili la watu wenye ulemavu. Aliongeza Ndugu Ramadhani Possi

Nae Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alimshukuru Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Ismail Msumi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kwa ajili ya kufanikisha swala la urejeshaji wa 10% kwa makundi hayo muhimu nakuwataka waendelee na utendaji huo.

Aidha Mh Mbunge aliongeza kwa kuwapongeza wanakikundi cha WAZALENDO kwa niaba ya vikundi vyote vilivyopokea mkopo na kuwataka kuhakikisha wanasimamia biashara zao vizuri na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili na vikundi vingine vinufaike kama wao walivyopata fedha hizo.

 

Serikali kupitia uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan inawapenda vijana na diomaana inaweka mkazo kwenye mikopo hiyo, hivyo kwa kutumia kipato watakachopata waimarisha Maisha yao kiuchumi, kwani hata katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha vitu vingi vimeshuka kwa lengo la kumuinua mwananchi maskini aweze kuimarika kimaisha na kiuchumi.

Mbunge wa jimbo la Chalinze alihitimisha kwa kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji Ndugu: Ramadhani Possi kuona namna ya kuwaongezea muda wa marejesho kwa mwezi mmoja kikundi hicho cha Wazalendo kwani tangu wamesaini mkataba wa kukabidhiwa mkopo huo umepita mwezi hadi kukabidhiwa vifaa hivyo, Kama kutahijika maamuzi ya vikao basi aone namna ya kuharakisha mchakato huo ili vijana waweze kunafaika zaidi kwa kupata muda wa kutosha kuvifanyia kazi vifaa kabla ya kuanza marejesho sawasawa na miongozo inavyotaka.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.