Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Halima Okashi akila kiapo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Omary Makame.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Hanji Godigodi akila kiapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Majid Mwanga akila kiapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mhe. Ngollo Malenya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku akitoa salamu za chama.
Baadhi ya wakurugenzi wakihudhuria hafla ya uapisho kwa Wakuu wa Wilaya.
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amewaapisha wakuu wapya wa wilaya ambao waliteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amewapa kazi ya kukabiliana na changamoto ya masuala ya migogoro ya ardhi kwenye wilaya zao pamoja na kutatua kero za Wananchi.
Wakuu hao wa wilaya ya Morogoro , Gairo, mvomero, Ulanga, Kilosa , Kilombero wameapishwa Juni 21/2021 ,sherehe ambazo zilifanyika katika Ikulu ndogo ya Mkoa wa Morogoro na kuhudhuriwa na watu wakiwemo watumishi mbalimbali, Viongozi wa dini, kisiasa, pamoja na wananchi.
RC Shigela, amewataka Wakuu hao wa wilaya kujenga mahusiano mazuri na chama na wasione kama kero pale wanapotakiwa kutoa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa ilani ya CCM.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando, amesema kuwa atahakikisha anasimamia sheria na utaratibu ili kutatua changamoto ili watu waweze kuishi kwenye mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao bila ya tatizo lolote.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Omary Makame,amesema kuwa atahakikisha uzalishaji mali unakuwa juu pamoja na kuhakikisha makusanyo ya Halmashauri yanakuwa juu ili kuharakisha maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mhe. Halima Okashi, amesema kuwa moja ni kutatua kero za wananchi ambazo wamepewa maelekezo na mkuu wa mkoa ikiwa ni pamoja na kutatua kero za wananchi na kubwa ni utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo imekithiri.
DC Okashi, amesema kuwa wataanza kutekeleza vipaumbele vya mkoa na atatumia vipaji na uwezo na mawazo yake ili kuleta maendeleo kwa kuleta mambo mapya ya kimaendeleo.
Naye mkuu wa wilaya ya Ulanga, Mhe. Ngollo Malenya ,amesema kuwa atashirikiana na wananchi wa Ulanga katika kutatua changamoto zao.
Hivi karibuni Rais aliteuwa wakuu wapya wa wilaya na kuwahamisha wale wa zamani kwenda maeneo mengine ambapo kwa wakuu wa wilaya aliohamihia mkoani wa Morogoro ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Morogoro, Ulanga, Mvomero, Kilombero, na Kilosa.
Post a Comment