RC SHIGELA ATOA NEEMA YA VIWANJA HEKARI 4500 WAKAZI WA KIEGEA STAR CITY MANISPAA YA MOROGORO
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela ,akisalimiana na mwananchi wa kiegea mara baada ya kumalizka kwa mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku, akisalimian ana wananchi wa kiegea Star City.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amegawa jumla ya hekari 4500 kwa wazaki wa Kiegea Manispaa ya Morogoro kufautia kutatauliwa mgogoro uliokuwa ukiwakabili baina yao pamoja na Mmiliki wa eneo hilo la Star City.
Hatua hiyo ya ugawaji wa hekari 4500 na kutatua mgogoro huo kwa wananchi, imefanyika Juni 18/2021 katika eneo la shamba hilo la Star City lililopo Kiegea Manispaa ya Morogoro.
Akziungumza na wananchi hao wakati wa mkutano wa hadhara wa kuongea na wananchi wanaotumia na kumiliki eneo hilo la Star City, juu ya muafaka wa mgogoro huo RC Shigela , amesema mgogoro huo umeisha na hataki kuusikia tena katika kichwa chake zaidi ya kutaka kuona maendeleo yanafanyika katika eneo hilo.
RC Shigela, amesema mgogoro huo ulidumu kwa muda mraefu lakini sasa ufumbuzi umepatikana na wananchi wamepatiwa hekari hizo ili waweze kufanya maendeleo.
Hata hivyo, amesema kuwa hataraijii kusikia tena mgogoro huo ukizungumziwa huku akiwataka wananchi wanaoishi katika shamba hilo wawe na subira wakisubiria Manispaa kuaandaa utaratibu wa kuweka muongozo mzuri wa kupima viwanja na jinsi ya kuweza kuupanga mji huo na kuweza kuonekana katika mpangilio mzuri.
" Mgogoro tumeumaliza, kilichobakia ni yale maamuzi ambayo tumekubaliana hapa ya Manispaa kuandaa mpango mzuri wa kupima maeneo na kuelekeza mambo ya kupanga mji vizuri , niwaombe sana wananchi tumemaliza mgogoro sitarajii kurudi tena hapa kutatua mgogoro nataka nikija tena nikute huduma za afya zipo, barabara nzuri na mpangilio mzuri wa makazi ili tuweze kusonga mbele katika kuelekea kuwa Jiji" Amesema RC Shigela.
‘’Narudia kusema nawashukuru sana wananchi wa eneo hili kwa kunisikiliza na hatimaye leo tumeweza kutatua kero za wananchi, kero ambayo miaka mingi imeshindikana, tumekuja tumefanya mkutano na mgogoro umeisha kwa maana ya kuoneshana maamuzi tuliyoafikiana tumeyapitisha kwa pamoja, " Ameongeza RC Shigela.
Sambamba na hayo, RC Sanare, ametoa onyo kwa wananchi wanaojimilikisha na kuuza ardhi nje ya taratibu zilizowekwa na Serikali na kuwataka kufuata sheria ili kuepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Katika utautzi wa mgogoro huo, maamuzi yaliyoafikiwa ni kwamba katika zoezi la kupima na kugawa ardhi , Manispaa ya Morogoro watanufaika kwa asilimia 45 huku wananchi wakinufaika kwa asilimia 55.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa eneo hilo la Kiegea Star City, akiwemo Bw, Anthony Hoza ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa huyo kwa kutatua mgogoro huo uliokuwa ukitishia Amani .
Naye, Fatma Athumani amesema mgogoro huo ulikuwa unamkosesha amani kutokana na uvamizi wa ardhi uliokuwepo ambao ulikuwa unapelekea ugomvi baina ya pande hizo mbili kwa maana ya wananchi wa mmiliki wa eneo hilo la Star City.
Mwisho, ameitaka Manispaa ya Morogoro,mara baada ya kutatua mgogoro huo kutenga Ardhi, kwa ajili ya huduma za jamii ikiwemo Shule, Afya, sehemu za kuzikia, michezo sehemu za kufanyia ibada n.k.
Post a Comment