MANISPAA YA MOROGORO YAMKABIDHI SHILINGI 300,000/= MKAZI WA KATA YA CHAMWINO ALIYEUNGULIWA NA NYUMBA.
MANISPAA ya Morogoro,
imemkabidhi Mkazi wa Kata ya Chamwino Mtaa wa Chamwino, Said Seif Mwele, kiasi cha
Shilingi 300,000/= kufuatia kuunguliwa na nyumba yake.
Akikabidhi fedha hizo kwa
niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Mchumi Manispaa ya Morogoro, Happines Masatu, amesema fedha hizo zimetolewa
kufuatia mkazi huyo kuunguliwa na nyumba na kupoteza mali zote.
Masatu , amesema baada ya
kupewa taarifa kupitia Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Ofisi ya Mkurugenzi
ilifika katika eneo hilo na kumuahidi mkazi huyo kumsaidia ili aendelee
kujikimu na maisha.
“Tulipokea taarifa kutoka kwa
Mtendaji wa Kata, ambapo mkazi huyo aliunguliwa na Nyumba tarehe 25 /09/2020 ,
baada ya taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro aliagiza kijana huyo
kupatiwa fedha ili aweze kujikimu kwani amepoteza kila kitu , kwahiyo leo
tumemkabidhi fedha aliyoahidiwa “ Amesema Masatu .
Kwa upande wa, Said Mwele, amemshukuru
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kuonyesha moyo wa kujali.
“Kweli nimepatwa na majanga
makubwa sana, lakini namshukuru sana Mkurugenzi wetu kwa kuonyesha kuguswa na
matatizo ya wananchi wake, hiki alichonipatia ni kikubwa kwangu kwani huu ni
msaada , naimani sasa nitavaa angalau nguo maana tangia tukio litokee sina nguo
za kubadili wala mahala kwa kulala ,
nina watoto 3 na mke wangu, kikubwa ni shukrani ni viongozi wachache wenye moyo
kama huu” Amesema Mwele.
Post a Comment