VIJANA WASOMI WATAKIWA KUFIKIRI ZAIDI KATIKA KUJIAJIRI.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa,akimkabidhi cheti mwanafunzi wa Chuo cha Mother Paula katika mahafali ya tatu ya chuo hicho.
Vijana Wasomi nchini Tanzania wametakiwa kuwa wabunifu na
kutumia usomi wao kutatua tatizo la ajira kwa kuacha kufikiria zaidi kuajiriwa
na Serikali au na makampuni makubwa na badala yake watumie fursa
zinazowazunguka zikiwemo kilimo,viwanda na biashara ili kuweza kujiajiri na
kujiatia kipato.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, Novemba 07, 2020 wakati wa Mahafali ya tatu ya Chuo cha Ufundi cha Mother Paula kilichopo Tarafa ya Mkuyuni Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, kuwa Serikali haiwezi kuajiri wasomi wanaohitimu kwenye vyuo vyote hapa nchini hivyo kuelekea uchumi wa viwanda vijana wasomi wanayo fursa ya kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato kupitia sekta ya viwanda.
DC Msulwa, amsema kuwa
wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknojia lazima vijana wabadilishe fikra
za kusubiri kuajiriwa na badala yake watafute maarifa ya kujiajiri.
Aidha, amesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda vijana
wanayo nafasi nzuri ya kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta ya viwanda,
kilimo, ufugaji, uvuvi na shughuli nyingine za ujasiliamali.
Kuhusu suala la changamoto ya mabweni shuleni, amesema kuwa tatizo hilo sio la Wilaya ya Morogoro pekee bali ni la nchi nzima ambapo kwa sasa Serikali ipo katika mipango ya kutengeneza mabweni katika Shule za Msingi na Sekondari ili kumlinda mototo wa kike.
“Swala la ulinzi kwa shule zetu hususani kwa Watoto wa kike ni changamoto sana, asilimia kubwa ya shule zetu za Msingi na Sekondari hazina mabweni, hivyo kwa sasa Serikali suala hilo lipo kwenye mpango ili kuwaokoa hawa watoto wetu waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea bila kukutana na vikwazo vyovyote mitaani” Amesema DC Msulwa.
Aidha, amesema amefurahishwa na masomo yanayotolewa hapo shuleni kwani yana lenga kuwasaidia wanafunzi wanapomaliza vyuo waweze kujitegemea na kuona mwanga wa ajira mbele yao.
“Kazi nimeona imefanyika na waalimu mnastahili pongezi kubwa sana, lakini nnipende kushauri ni vizuri kuangalia mitaala ya elimu, kwani sasa hivi wanafunzi wanatakiwa wasome kulingana na soko la ajira lililopo, unaweza kuona unawafundisha wanafunzi lakini wanapofika mitaani wakakutana na uhalisia wa maisha wakajuta na kuona vyuoni wamepoteza muda, kwahiyo Serikali haiwezi kuajiri wanafunzi wote lakini inachoweza kufanya Serikali ni kutengeneza mazingira mazuri yatakayoweza kuwafanya wananfunzi waweze kijitegemea,
DC Msulwa, ametaka somo la utalii lipewe kipaumbele kwani sasa Mji unakuwa kwa kasi hivyo lazima kuzalisha watu wazuri wanaoweza kutoa huduma bora katika vivutio vya utalii ikiwamo na huduma za Hoteli.
Katika hatua nyengine, amewataka wakuu wa Shule wanapofanya mahafali kama hayo wawaalike wataalamu kutoka taaisis mbalimbali ikiwamo Maafisa Maendeo ya Jamii za Halmashauri pamoja na wamiliki wa Taasisi ili waweze kuwasaidia kupata uzoefu na kuwasaidia wale wanafunzi wanaohitimu masomo yao.
Amesema Halmashauri kuna mikopo inayotolewa hivyo kama maandiko yatafundishwa shuleni ni wazi kuwa wanafunzi watakuwa na uelewa mkubwa na wataweza kukaa katika vikundi kuandika andiko la biashara ili kuweza kupata mikopo kwa kuwa watakuwa na taaluma zao za ustadi wa maisha.
Post a Comment