Header Ads

WANANCHI WA MANISPAA YA MOROGORO WATAKIWA KUPINGA VITA UKATILI DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

 

WANANCHI wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wametakiwa kupinga vita dhidi ya unyanyasaji wa Kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, wakati wa Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia.

Akizungumza juu ya siku 16 za kupinga vita dhidi ya ukatili wa kijinsia, amesema kuwa suala la Msingi ni kuendeleza mshikamano katika malezi ya watoto ili kuweza kuwalinda na kuwawekea mazingira salama hasa watoto wa kike ili kuweza kuwaondoa kwenye hatari ya kukabiliana na vitendo vya ubakaji na ulawiti.

“Kumekuwa na  matukio mabaya sana vitendo vya kiukatili ikiwemo kuwabaka na kuwalawiti, hali hii haikubaliki lazima wale wanaojihusha na matendo kama haya wachukuliwe hatua kali za kisheria, kwahiyo niwaombe Wananchi wa Manispaa ya Morogoro tunapoelekea kuadhimisha siku 16 za kupinga vita dhidi ya ukatili wa kijinsia tuhakikishe Watoto wetu wanakuwa salama , wanapatiwa elimu ya kutosha pamoja na kuwa karibu na Wazazi na kuwafundisha jinsi ya kutoa taarifa mara wanapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji pamoja na wananchi kujenga utamaduni kutoa taarifa ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo.” Amesema Lukuba.

Mwisho, ameendelea  kusisitiza kuwa wakati huu wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ni vizuri kuendelea kuweka mkakati wa kutosha ili kuweza kuwadhibiti wale  wanaoendeleza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa upande wa Matibu wa dawati la maendeleo ya mtoto,tupinge ukatili wa kijinsia mabadiliko yanaanza na mimi

Kwa upande wa Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Mtoto Manispaa ya Morogoro, Joyce Mugambi, amewataka Wananchi kujenga utamaduni wa kutoa taarifa ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo.

Amesema katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wameanza kutoa elimu katika vyombo vya habari pamoja na Shuleni.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.