Header Ads

TANGAZO MAADHIMISHO YA WIKI YA KUZUIA NA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA DUNIANI


 MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro anawatangazia Wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro kuwa kuanzia tarehe 10-14 Novemba 2020, kutakuwa na maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCD).

Huduma mbali mbali za uchunguzi , Ushauri na  Elimu zitatolewa kuhusiana na magonjwa yafuatayo;

  • Shinikizo la damu
  • Kisukari
  • Saratani ya shingo/mlango wa kizazi
  • Lishe
  • Afya ya akili
Huduma zitatolewa kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9:30 mchana katika kituo cha Afya Sabasaba.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.