DC MSULWA KUANZISHA WIKI YA MAONESHO YA WAJASIRIAMALI WILAYA YA MOROGORO.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akizungumza na Wajasiriamali kwenye hafla ya uzinduzi wa Mgahawa wa Mji Kasoro.
Mkurugenzi wa Mji Kasoro, Zena Mng'ong'o (kulia) wakigonga chiazi na Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akikata keki.
Afisa Utamaduni Manispaa ya Morogoro, Safia Kingwah, akifungua shampeni .
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amesema atahakikisha anafungua wiki ya maonesho kwa Wajasiriamali ili kutangaza bidhaa zao na kunyanyua kipato.
Kauli hiyo, ameitoa Novemba 07,2020, wakati wa uzinduzi wa Mgahawa ujulikanao kwa jina la Mji Kasoro uliopo Savoy Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kuwa, lengo hasa la maonesho hayo ni kuwapa fursa wafanyabiashara kuonesha bidhaa zao na si kuuza, ili wanapomaliza maonesho wapate wateja na fursa pana zaidi za kibiashara.
Aidha, amesema kuwa, maonesho hayo yatalenga zaidi kusaidia wajasiriamali wadogo ili kuifikisha Tanzania katika uchumi wa viwanda.
"''Tunaamini biashara ndiyo inayokuza viwanda na bila kuuza hakuna ukuaji wa viwanda, hivyo basi kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote tutaandaa siku ya Wajasiriamali Wilaya ya Morogoro ili kila Mjasiriamali aweze kutangaza bidhaa zake, lazima tujifunze kutangaza vya kwetu, tusisubiri mpaka maonesho ya nanenane ndio tutatangaze tutachelewa sana , ni suala la muda ngoja tujipange hakuna kitakachoshindikana , tunapoelekea ni pazuri tunahitaji kuwa Jiji sasa hatuwezi kuwa Jiji kama hatuna wajasiriamali wakutosha wakututengenezea bidhaa, tutapokea wageni na mtauza lakini bidhaa zetu lazima ziwe bora tunahitaji Morogoro ya Viwango tukianza na nyinyi" Amesema DC Msulwa.
Hata hivyo, amewataka watakao shiriki watumie maonesho hayo kutangaza bidhaa zao badala ya kufikiria kuuza, lakini pia wabadilishane ujuzi na uzoefu na wafanyabiashara wa kimataifa.
Kwa upande wa Mmiliki wa Mgahawa huo, Bi Zena Mng'ong'o ,amesema kuwa huduma zinazotolewa hapo zitazingatia ubora wa hali ya juu.
"Namshukuru sana Mkuu wetu wa Wilaya kuja kushiriki na sisi, hii imenipa faraja kubwa kuona Viongozi wetu wakituunga mkono, tupo tayari kushirikiana na Viongozi wa Serikali kwani wao ndio wamebeba maono ya Taifa hili, lakini nampongeza sana Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kweli ni mama mchapa kazi, amekuja kwa muda mchache lakini maendeleo yake ni makubwa sana , wanawake tukiwezeshwa tunaweza , tunamuomba Mhe. Rais azidi kutuamini ili tulifikishe Taifa hili mbele kimaendeleo'Amesema Bi. Zana.
Post a Comment