TANGAZO OFISI YA MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO KUELEKEA WIKI YA USAFI WA MAZINGIRA NA SIKU YA MATUMIZI YA CHOO DUNIANI.
MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOROGORO ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA KUANZIA TAREHE 16 HADI TAREHE 19 MWEZI WA 11 ,2020 NI WIKI YA USAFI WA MAZINGIRA NA TAREHE 19 NI SIKU YA MATUMIZI YA CHOO DUNIANI KILA MWAKA HIVYO WANANCHI WANATAKIWA KUFANYA YAFUATAYO;
- WEKA CHOMBO CHA KUNAWIA MIKONO UTOKAPO CHOONI NA NAWA MIKONO YAKO MARA KWA MARA KWA MAJI SAFI TIRIRIKA NA SABUNI.
- JENGA CHOO BORA KIWE CHA KUDUMU.
- SAFISHA MAZINGIRA YANAYOKUZUNGUKA KWA KUF
YEKA NYASI, KULIMA NA KUFUKIA MADIMBWI YASIYOHUSIKA .
- MAMA LISHE, BABA LISHE,BAR, NYUMBA ZA WAGENI (GUEST HOUSE),HOTELI,VIBANDA VYA BIASHARA FUATA MAAGIZO YA KIAFYA YATOLEWAYO NA WATAALAMU WA AFYA.
KUMBUKA
UKAGUZI UTAPITA NA HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAKO UTAKAYEKAIDI MAAGIZO HAYO.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO KWA KUSHIRIKIANA NA MKOA, WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.
KAULI MBIU: 'ZINGATIA MAHITAJI YA JINSIA KWA USAFI WA MAZINGIRA ENDELEVU'.
TA
Post a Comment