Header Ads

DC MSULWA AZINDUA STENDI YA KALOLENI MANISPAA YA MOROGORO HUKU AKIWATAKA WANANCHI KUITUNZA MIUNDOMBINU ILIYOPO.

 

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (kulia) baada ya kuzindua  Stendi ya Daladala ya Kaloleni, (kushoto) Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Michael Waluse.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (kulia), akiwa amekata utepe kuashiria zoezi la kuzinduliwa kwa Stendi ya Daladala ya Kaloleni likiwa limekamilika.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa (kulia),akikata utepe kuashiria zoezi la uzinduzi wa  Stendi ya Daladala Kaloleni limefanyika, (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Michael Waluse.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, (kushoto) akisalimiana na Afisa Utumishi, Shabani Duru, mara baada ya kuwasili katika Stendi ya Daladala Kaloleni.(kushoto) Afisa Ugavi na manunuzi Manispaa ya Morogoro, Jafari Makupula, Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro James Mnene pamoja na Mkguzi wa ndani Manispaa ya Morogoro Neema Dachi.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse (katikati) akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Wilaya wakati wa zoezi la kukgaua Stendi.

Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro, James Mnene (kushoto ya DC ) wakiteta jambo na Mkuu wa Wilaya wakati wa zoezi la kukgua Stendi hiyo. 

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa akizungumza na Wananchi wakati wa uzinduzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni.



Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro, James Mnene, akisoma taarifa ya Ujenzi wa stendi ya Daladala ya Kaloleni mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Stendi hiyo.
Diwani mteule wa Kata ya Mji Mpya, Emmy Kiula, akitoa salama za Wananchi wa Kta ya Mji Mpya mbele ya Mkuu wa Wilaya.


MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewataka Wananchi kutunza miundombinu iliyopo katika maeneo yao kwa sababu matengenezo yao yanatokana na kodi zao.

Kauli hiyo emeitoa leo Novemba 06/2020,  wakati wa Uzinduzi wa Stendi ya Daladala ya Kaloleni iliyopo Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro.

Msulwa, amesema kuwa licha ya kuwa haki yao, njia moja wapo ya kuthamini fedha zao ni kulinda miundombinu iliyopo na inayoendelea kujengwa.

“Tatizo kubwa tulilo nalo ni kushindwa kutambua haki na wajibu wetu kama walaji, hiyo ndiyo sababu inayotufanya kugharamia vitu ambavyo kama tungevitunza vizuri tusingetarajia kupata gharama hizo, kwahiyo ni wajibu wetu kuthamini fedha zetu maaana zinatokana na kodi zetu wenyewe “ Ameongeza DC Msulwa.

 “Manispaa ya Morogoro ni Mji Kongwe sana , kwa hili lililofanyika leo naupongeza sana Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa kuonesha na kuufanya Mji huu  kuwa  sura ya Manispaa, lakini niseme unapokuwa na Uongozi mzuri ngazi ya Kitaifa, Jimbo na Kata unatengeneza uelekeo mzuri wa kutengeneza maendeleo kwa wananchi au taasisi husika, kwahiyo uchaguzi umekwisha, matokeo tumeyasikia na  Viongozi wetu wameshaanza kufanya kazi lakini tunasubiria wapishwe ili waweze kujipanga vizuri ” Amesema Msulwa.

Aidha, amesema lengo la Manispaa hii ni kuwa Jiji hivyo ni lazima miundombinu iweze kuboreshwa licha ya kuwa zipo changamoto zitakazo jitokeza.

“”Hatuwezi kukaa katika Manispaa kwa miaka 32 na tukaendelea kukaa kwa muda mrefu kabla ya hatujafika kiwango cha kuwa Jiji, lakini ukishakuwa Jiji lazima utarajie changamoto mbalimbali, changamoto hizo pia zinaweza kugeuka kuwa fursa , kwahiyo hatua ambazo Manispaa imezichukua zinatufanya kuelekea kuwa Jiji, nafahamu ukiachia stendi hii ya Kaloleni, kuna Stendi kuu ya Daladala Mafiga, Soko Kuu la Kisasa, na miradi mingene ambayo inaendelea nawapongeza sana Manispaa, Wahandisi  wa miradi kwa kazi kubwa na nzuri mnazo fanya,””Ameongeza DC Msulwa. 

Pamoja na hayo amesema ni vizuri pia Mkurugenzi wa Morogoro Vijijini kufika hapa na timu yake ya Uongozi ili nao waweze kujifunza na wao wakajenge Stendi kama hii kwa ajili ya kurahisisha huduma za usafiri kwa Wananchi wao.

Mwisho , DC Msulwa, ameahidi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya ukarabati wa Kituo kidogo cha Polisi cha Mji Mpya.

Naye Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, mbali na kushukuru kwa pongezi zilizotolewa katika ofisi yake, ameahidi kushirikiana na Uongozi wa Daladala wa Stendi hiyo kwa yale yote yatakayojitokeza kuhusiana na Stendi hiyo.

Waluse, amesema kuhusu Ukarabati wa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo jirani na Stendi hiyo, katika vikao watajadili na kuona ni jinsi gani Manispaa itakavyoweza kushiriki katika hatua hiyo ya ukarabati ili iendane na hadhi ya Stendi hiyo kwani Jeshi la Polisi ndio watu wa kwanza katika kulinda amani katika eneo hilo.

Kwa upande wa Msimamizi wa fedha za mkopo wa Benki ya Dunia chini ya fedha za  uboreshaji Miji ( Urban Local Government Strengthening Program (ULGSP) na Mhandisi wa TARURA Manispaa ya Morogoro, James Mnene, amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 644 ambapo ujenzi wake ulianza Aprili 28/2020.

Mnene, amesema mkandarasi Nandhra amekamilisha Ujenzi huo kwa asilimia mia moja kama ilivyoonekana wakati wa ukaguzi kabla ya kuzinuduliwa.

“”Mradi umekamilika kwa silimia mia moja kama mnavyoona,lakini kazi ambayo imebakia ni kuweka alama za kuongoza magari lakini kazi hizi zote zitafanyika katika kipindi cha matazamio,mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa shilingi milioni 566 sawa na asilimia 74.9 na kiasi kilichobakia atalipwa baada ya kuwasilisha madai yake ya mwishoni  na matumaini ya Manispaa ya Morogoro katika Stendi hii ya Daladala ni kutoa huduma bora ya usafiri kwa magari ya Daladala yapatao 50 na kuongeza Manispaa mapato na hadi sasa hakuna kipingamizi chcochote cha kutofanya stendi hii kutotumika “ Amesema Mnene.

Hata hivyo, Diwani mteule wa Kata ya Mji Mpya, Emmy Kiula, amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Bakari Msulwa , kwa kukubali ombi lake la kukarabati Kituo kidogo cha Polisi cha Kata ya Mji Mpya kufuatia Mkuu wa Wilaya kuahidi kiasi cha Shilingi Milioni moja.

Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Daladala Mkoa wa Morogoro, Hemed Ntengwa, amesema Stendi hiyo ilikuwa changamoto sana lakini kwa sasa watafanya kazi vizuri na kuitunza miundombinu ya Stendi hiyo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.