Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAANZA KUTOA ELIMU KATIKA MAKUNDI MBALI MBALI JUU YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA LEO NOVEMBA 26/2020.

Miongoni mwa makundi yaliyofikiwa kupatiwa elimu leo Novemba 26/2020  dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na kupinga vita dhidi ya ukatili wa kijinsia ni pamoja na Shuleni , Vijiwe vya bodaboda, Bajaji vilivyopo JUWATA , pamoja na wauza mboga mboga.
Elimu hiyo itaendela katika Shule mbalimbali za Msingi na sehemu zenye mikusanyiko ya watu hadi Siku ya mwisho ambayo ndiyo kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo Kimkoa yanaadhimishwa Manispaa ya Morogoro kwenye Stendi Mpya ya Daladala Mafiga .
KAULI MBIU: MSHIKAMANO WA KIMATAIFA , TUWAJIBIKE  KWA PAMOJA' 

Pia katika maadhimisho hayo, magonjwa yasiyoambukiza na ya kuambukizwa yatapimwa bila malipo kuanzia Tarehe 29-01 Desemba 2020.
Siku 16 za kupinga vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia umeanza tarehe 25 hadi Desemba 10, 2020 ambapo kauli mbiu inasema : TUPINGE UKATILI WA KIJINSIA:MABADILIKO YANAANZA NA MIMI'.


Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Manispaa ya Morogoro, Upendo Elias akitoa elimu juu ya kujikinga na virusi vya UKIMWI kwa Wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita  Shule ya Sekondari Morogoro leo Novemba 26/2020 wakati wa kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika Tarehe 1 Desemba 2020 kwenye Stendi Mpya ya Daladala Mafiga.
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini elimu inayotolewa na Wataalamu kutoka Manispaa ya Morogoro.




Mratibu wa TASAF, Feliciana Katemana, akiendelea kutoa elimu dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia. 
















 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.