Header Ads

KASI YA UJENZI WA SGR KITUO CHA MOROGORO WAMKUNA WAZIRI MAJALIWA.


 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (katikati) , akizungumza mara baada ya kuwasili kwenye Kituo kikubwa cha Reli ya kisasa kilichopo Manispaa ya Morogoro eneo la Kilimanjaro kata ya Kihonda.(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare. 

Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro, Ruth John (kushoto), Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba (katikati), Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma (kulia) wakiteta jambo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo Novemba 18/2020 kwenye Kituo kikubwa cha mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR).



WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa Reli ya mwendokasi unaoendelea katika Kituo kikubwa cha Morogoro.

Kauli hiyo ,ameitoaleo Novemba 18/2020 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho  kukamilika kwa usafiri wa Dar Es Salaam hadi Morogoro.

Majiliwa, amesema ndoto za Mhe. Dkt. John Magufuli, za kuhakikisha miradi hii mikubwa inakwenda kuwa na tija zinaelekea kukamilika.

Aidha, amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)  huku akisema kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni inayojenga mradi huo hatua zilizobakia katika kituo hicho  ni suala la kuunganisha umeme katika baadhi ya maeneo ili kazi zianze.

 ‘”Mradi wetu unaendelea vizuri sana, tunashukuru kampuni yetu ya Yapi Merkezi inafanya kazi nzuri sana, leo nimekuja kukagua kituo kikubwa cha hapa Morogoro,  nilishafanya  hivyo Dar Es Salaam kwenye lile Jengo letu la  Tanzanite, nimefanya hivyo kwenye Karakana yetu kubwa ya Soga , na baadae nilipanda Treni kuanzia Soga mpaka Pugu, na sasa Mkurugenzi ananiambia tunaweza kupanda Treni kuanzia huko mpaka kilomita 150 hapa katikati hivyo zimebakia kilomita 50 mpaka 60 kufika Morogoro ili tuanze kutembea kwa Reli”Amesema Majaliwa.

Hata hivyo, amesema kuwa mradi huo ulitakiwa kukamilika mwezi Desemba lakini matarajio yaliyopo hadi kufikia mwezi Aprili mwakani  Reli hiyo itaanza kazi.

“”Awali tulikuwa tumalize mwishoni mwa Desemba hii  2019, lakini mnajua tulipatwa na tatizo duniani la ugonjwa wa Corona , na baadhi ya vifaa vingi vinatoka nje nako kuna magonjwa yanaendelea , kwahiyo usafirishaji wa mizigo na ujaji wa wataalamu tulichelewa sana lakini hata hivyo kuchelewa kwao hakuja athiri mwenendo wa mradi kwani taarifa zao zinaendana na matamanio na malengo yetu “ Ameongeza Mhe. Majaliwa.

Katika hatua nyengine, amesema uwepo wa mradi huo umeongeza kiwango cha ajira kwani imeajiri vijana wengi wanaofanya kazi katika mradi huo.

Amesema miongoni mwa malengo makubwa ya Serikali kujenga miradi mikubwa kama hii ni pamoja na kuleta ajira ili kuwafanya Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa miundombinu hii mikubwa inayoleta faida hapa nchini pamoja na kujenga uchumi wa nchi.

Waziri Majaliwa, amewataka vijana waliobahatika kufanya kazi katika miradi hiyo mikubwa wahakikishe wanabeba utaaamu na ujuzi  mbalimbali ili waweze kufanya kazi vizuri ya kuendesha hiyo miradi  mara baada ya wataalamu hao kukamilisha miradi na kurudi makwao.

Mwisho amewaondoa wasiwasi na kujaza matumaini Uongozi wa  Manispaa ya Morogoro huku akisema ile hamu ya kuwa Jiji itafikiwa na malengo yatafanikiwa kikubwa ni kuonesha jinsi walivyojipanga kukabilioana kuwa Jiji na ifikapo tarehe 28 Novemba mwaka 2020 wawasili  Dodoma tayari kwa mazungumzo ya awali.

Ziara hiyo ya Waziri Majaliwa, imeendelea tena kwenye ukaguzi wa mradi wa ufuaji wa umeme kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.

 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.