Header Ads

RC SANARE AWATAKA WAZAZI KUFANYIA KAZI KWA VITENDO MAAZIMIO YA VIKAO VYA KAMATI ZA SHULE.

 







MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare,amewataka Wazazi  kufanyia kazi kwa vitendo maazimio mbalimbali  yanayotolewa katika Vikao vya Kamati za Shule ili kuinua ubora wa Elimu.

Hayo ameyasema leo Septemba 28,2020 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Madarasa wa Shule ya Msingi Juhudi Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Sanare, amewataka Wazazi kuwa mstari wa mbele katika kutimiza maagizo na yatokanayo yote yaliyojadiliwa katika vikao vya Kamati za shule ili kuweza kuinua ubora wa elimu .

RC Sanare, amesema ni muhimu kwa Wazazi wanaoshiriki  katika Vikao vya kamati za shule  kuyachukua maazimio yatokanayo na kikao katika kutekeleza kwa Vitendo yale yaliyoazimiwa jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta ya Elimu.

"Nimeona nifike hapa tujadili kwa pamoja ili Kudumisha Ushirikiano baina ya Walimu na Wazazi katika kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu ikiwemo utoaji wa chakula inapatiwa ufumbuzi ikiwamo uzingatiaji  utoaji wa Elimu ya awali,Uboreshaji wa miundombinu pamoja na kuzingatia utekelezaji wa maazimio yanayotokana na Kamati  za shule, niwaombe Wazazi hawa ni watoto wetu wanahitaji elimu  bora sasa kama sisi tutakwama hata elimu bora hawa watoto watakosa Serikali inafanya kazi kubwa ya kuimarisha elimu yetu kwa Watoto lakini kama wazazi pia tunayo majukumu ya kufanya kwa upande wetu ikiwamo kuchangia katika ujenzi na michango ya Chakula kwa Watoto wetu wawapo shuleni na ujenzi wa madarasa " Amesema RC Sanare .

Hata hivyo, katika kuhakikisha Ujenzi wa Madarasa 3 yaliyobakia yanakamilika , amesema kupitia Ofisi yake kushirikiana na  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, kuchangia kiasi cha Shilingi milioni 20 ambapo milioni 17 zilizobakia Wazazi watachangia kwakuwa hadi hatua iliyopo nguvu zote zimetoka Serikalini.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewataka  Wazazi wa Wanafunzi  kujitoa kwa moyo kuchangia Chakula Shuleni ili kuwawezesha watoto kupata chakula cha kutosha jambo litalaowawezesha watoto hao kuwa na Afya nzuri hali itakayowaezesha kufanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuinua ubora wa Elimu .


DC Msulwa, amewataka Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Walimu ikiwa ni sambamba na kujenga mazingira mazuri yatayowezesha Walimu na Watumishi katika Sekta ya Elimu kupenda mazingira ya kazi jambo litakalosaidia kuinua ubora wa Elimu.

 Shule ya Juhudi ni miongoni mwa shule pacha ya msingi Lukobe ambayo mpaaka sasa ina jumla ya madarasa 3 yaliyomaliziwa na Wanafunzi wanasoma ambapo madarasa 3 yapo katika hatua ya upauaji .


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.