RC SANARE AWATAKA WAZAZI NA WAALIMU KUSHIRIKIANA ILI KUONGEZA VIWANGO VYA UFAULU.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare akiwa pamoja na Wanafunzi wa Chekechea mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mkutano Shule ya Msingi Chief Albert. |
WAZAZI na Walimu wametakiwa kushiriana kwa
karibu ili kwa kuweza kuinua taaluma ya watoto wawapo mashuleni na hivyo
kuwajengea msingi ulio bora katika maisha yao ya kila siku.
Hayo ameyasema leo Septemba 08,2020 wakati wa
ziara ya kukagua maendeleo ya Shule ya Msingi Chief Albert , iliyopo Kata ya
Mindu Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa
habari, RC Sanare, amesema wazazi ni nguzo ya kwanza kwa watoto na ili
wafanikiwa ni lazima wanapowapeleka shuleni wahakikishe wanashirikiana na
walimu wa watoto hao kikamilifu.
Aidha RC Sanare, ameipongeza
shule hiyo kwa kuwa mfano bora kwa upande wa TEHAMA kwa Shule za Msingi Mkoani
Morogoro huku akiwaagiza Maafisa Elimu Msingi wote kuhakikisha wanakuwa na
mipango endelevu ya kuona kila Shule inakuwa na Chumba cha Kompyuta na kuwa na
vifaa vya kutosha ili waanze kuwakuza Watoto katika msingi mzuri juu ya somo la
TEHAMA.
RC
Sanare, amebainisha kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vema kila wakati kwa kuwa
walimu wamekuwa mstari wa mbele katika ufundishaji ulio bora unaofanya mtoto
anapokuja shule hiyo anaonesha mabadiliko muda mfupi na hiyo ni sababu ya
uangalizi bora wa walimu hao kwa watoto.
Lakini kwa mujibu
wa taarifa iliyosomwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Chief Albert, Mwl.
Theresia Swai, amesema kuwa ufaulu wa Shule hiyo umekuwa ukiridhisha na kusema
kuwa hii inamaanisha watoto hao ni zao jema katika maisha ya baadaye endapo
wazazi wataendelea kuzingatia kuwafuatilia kwa ukaribu.
“ Viwango vya ufaulu vinakuja kutokana na Ushirikiano mzuri
wa Wazazi na Waalimu, kwahiyo lazima mtambue kuwa wazazi wanafanya kazi nzuri
kwa kuwaandaa watoto wao katika ujenzi wa Taifa kwani mchango wao ni Asilimia
25 hivyo wasijisahau kuona umuhimu kuwalipia chakula cha mchana kwani
inamsaidia kumfanya mtoto awe makini darasani pasipo kushinda na njaa” Amesema
RC Sanare.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amesisitiza ushirikiano huku
akiwataka Waalimu na Wazazi washirikiane vizuri na wasiwe sehemu ya matatizo
kwani kufanya hivyo kunafifiza ufaulu kwa wanafunzi wao.
“Nimepokea
maagizo kwa Kiongozi wangu wa Mkoa, nitayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ,
lakini Wazazi na Waalimu tusiwe sehemu ya matatizo, tushikamane kwa kila jambo,
haya yote niliyoyasikia na kuagizwa Jumamosi asubuhi nitafika hapa tuzungumze
na Wananchi kwanza baada ya hapo tutakaa na kamati ya shule (Wazazi) na Waalimu
ili tuone tunatatua vipi hizi changamoto, tukitoka hapo tusitafute mchawi tuwe
wamoja kwa ajili ya kusukuma gurudumu mbele la taaluma katika Manispaa yetu na
Wilaya yetu kwa ujumla”Amesema DC Msulwa.
Upande
wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chief Albert, amesema kuwa mategemeo ya shule ni kuwasaidia watoto hasa
wa darasa la saba mwakani kuweza kufika nafasi za juu kitaaluma.
Aidha,
Bi Theresia ametoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya , Katibu
Tawala , Kaimu Mkurugenzi na wengine wote waliofika na kuungana na uongozi wa
shule na kusema hali hiyo inaonesha wote ni wamoja.
Post a Comment