Milioni 214 kutolewa kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu Manispaa ya Morogoro.
HALMASHAURI
ya Manispaa ya Morogoro inatarajia kutoa
zaidi ya Shilingi milioni 214 kwa ajili
ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Kauli
hiyo imetolewa leo Septemba 17,2020 na Afisa Afisa Maendeleo ya Jamii, Enedy Mwanakatwe, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro wakati wa zoezi la Utiaji wa
saini kwa Wawakilishi wa vikundi hivyo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Mwanakatwe, amesema jumla ya Vikundi 13 vinatarajiwa
kunufaika na fedha hizo zinazotolewa na
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo fedha hizo ni sehemu ya asilimia 10 ya
Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha,
katika hatua nyengine, vikundi hivyo leo vilikuwa katika zoezi la utiaji wa
saini pamoja na semina ya kanuni za Utoaji na usimamizi wa mikopo kwa Vikundi
vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambapo semina hiyo iliendeshwa na
Mwanasheria wa Manispaa ya Morogoro, Elikarimu Tyeah.
“Leo
ni siku ya pili ya mafunzo yetu ya
ujasiriamali kwa walengwa wa mikopo ,
tunatarajia kutoa mikopo kwa fedha shilingi milioni 241,490,000/= zilizobakia katika bajeti yetu ya mwaka wa
jana 2019/2020 kabla ya mwaka huu wa
fedha lakini tumeona tuanze na mafunzo kama sheria inavyosema ili walengwa wetu
wawe na ufahamu mkuwa tukiwa lengo kuwawezesha wanawake, watu wenye ulemavu na
vijana na jamii kwa ujumla kuweza kujiajiri. kuwafanya wanawake na vijana
watambue wajibu wao katika kujiletea maendeleo na kuifanya jamii kutambua fursa
mbalimbali zilizo za halali katika maeneo yanayowazunguka,” Amesema Mwanakatwe.
“Bajeti
iliyopita katika mapato yetu ya ndani ya asilimia 10 tulishatoa mikopo kwa
vikundi vingi sana na mpaka sasa vikundi vimeweza kujipatia maendelo ya wao
wenyewe kwa kufanya biashara ndogondogo na hivyo wameweza kujikimu katika
malazi, chakula na mavazi. wanawake, walemavu na vijana wa Manispaa ya Morogoro
wanaheshimika kwa kuwa sasa wanao uwezo
wa kufanya biashara na kupata fedha za kujikimu” Ameongeza Mwanakatwe.
Mwisho,
Mwanakatwe, ametoa rai kwa Walengwa hao wa mikopo kuwa fedha wanazopatiwa sio
msaada bali zinatakiwa kurejeshwa kwa wakati na kuzifanyia shughuli zilizokusudiwa
kwa ajili ya kujiletea maendeleo binanfsi na Taifa kwa ujumla.
Naye
Mwanasheria wa Manispaa ya Morogoro, Elikarimu Tyeah, amesema kuwa fedha watakazokopeshwa wanapaswa kuzitumia katika malengo waliyoombea
na siyo kupeleka katika matumizi mengine kama vile starehe na anasa ambazo
zitawafanya washindwe kurejesha.
“”Leo tumesaini mikataba, mtambue hizi ni fedha ambazo
zinahitaji mzunguko, sio unapata unazitumia kwa ajili ya starehe kwakweli
tutafikishana Mahakamani na tutawafunga, kikubwa baada ya kupata fedha hizi
zitumike katika malengo yaliyokusudiwa ilia zirejeshwe kwa wakati na wengine
waweze kuapatiwa, tuzingatie sheria na kanuni , tukifanya hivyo tutakuwa watu wema
na tutaendelea kuaminika zaidi na kupata mikopo zaidi ya hapa na kubadilisha
maisha yetu na kuchangia pato la Taifa hususani katika kuelekea Tanzania ya
Viwanda na Uchumi wa wakati ambapo kwa sasa tumefikia””Amesema Elikarimu.
Katika Mwaka wa fedha wa 2019/2020 Manispaa ya Morogoro ilitoa jumala ya shilingi milioni 517,800,000/= kwa ajili ya mikopo ya uwezeshaji kwa vikundi 72, ikihusisha vikundi 44 vya wanawake na vikundi 22 vya vijana pamoja na Vikundi 6 vya Watu wenye Ulemavu.
Ikumbukwe
kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, katika utekelezaji wa bajeti yake kila mwaka
imekuwa ikitenga asilimia 10 ya Mapato
ya ndani kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake asilimia 4,Vijana asilimia 4 na asilimia
2 kwa Watu wenye Ulemavu.
Post a Comment