MANISPAA YA MOROGORO YADHAMIRIA KUTEKELEZA MIRADI KWA VIWANGO VINAVYOSTAHILI.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse (wapili kutoka kushoto) akiwa na timu ya Wataalamu wakikagua Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Mkundi (kushoto) Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro, Pili Kitwana.
Wajumbe wa C.M.T Manispaa ya Morogoro wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Michael Waluse wakijadiliana mara baada ya kufika katika Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Luhungo.
Ujenzi wa Ofisi ya Kata Luhungo ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika.
Wajumbe wa C.M.T wakipata maelezo juu ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Sina Kata ya Mafisa.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro katika kuona inakuwa na miradi yenye matokeo chanya, imedhamiria kutekeleza miradi yote iliyopo kwa viwango vinavyostahili ili kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 10, 2020 na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyomalizika na inayoendelea .
Akizungumza na Waandishi wa habari, Waluse, amesema lengo la ziara ya leo ni kuhakikisha miradi yote inakamilishwa kwa viwango vinavyostahili na kuonesha thamani ya fedha inayotumika katika miradi hiyo ikiwa ni moja ya uwajibikaji na usimamizi bora kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wananchi.
Aidha,
amesema kuwa Matokeo chanya katika uwajibikaji,usimimamizi mzuri na uwazi kwa
serikali ya awamu ya tano, umeiwezesha Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutekeleza
mradi mikubwa ikiwamo mradi wa Ujenzi wa Soko Kuu la Kisasa , mradi wa Ujenzi
wa Stendi Mpya ya Dalala Mafiga, Stendi ya Kaloleni, mradi wa Kitega Uchumi DDC ,
ukamilishaji wa Maboma ya Shule na Ujenzi mpya wa Madarasa , Ujenzi wa Barabara
pamoja na Ujenzi wa Ofisi za Kata.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi, Waluse, amesema ziara hiyo ni
utaratibu wa kawaida ambapo Wajumbe wa C.M.T wamekuwa wakiufanya wa kutembelea
miradi hiyo badala ya kusubiria taarifa mezani jambo ambalo linashindwa kufanya
maamuzi sahihi yanayokusudiwa.
“Katika
utawala wa serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Dk.John Magufuli, kuna
miradi mingi ambayo tumeikamilisha na mingine bado inaendelea, lakini katika
miradi hiyo ipo ambayo tumeitekeleza kwa kutumia mapato yetu ya ndani na
mingine ni fedha kutoka Serikali kuu ikiwamo mradi wa Stendi ya Daladala, Soko
, hivyo katika kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa ufanisi wa viwango vya
juu tumeona tutembelee tuione kwa macho kitu gani tukifanye ili miradi hii
ikamilike na hata katika vikao vyetu
tunapokwenda kufanya maamuzi tufanye maamuzi yanayostahili kuliko kusubiria
taarifa mezani, miradi inaridhisha sana Ofisi za Kata nzuri, Maboma ya shule
yamekamilisha bado umaliziaji ambao unaendelea, tunaamini baada ya muda miradi
hii itakamilika ili kuweza kutoa huduma kwa jamii, “ Amesema Waluse.
Waluse,
amewaomba Wananchi wasikae mbali na Serikali yao kwani wanatakiwa kushiriki
katika kuchangaia miradi ya maendeleo.
“”Tumeona
kuna ujenzi wa Madarasa lakini niwaombe Wazazi na Kamati za Shule wawekeze
nguvu katika kuanzisha ujenzi wa Vyumba vya Mdarasa baada ya hapo Manispaa
tutatina nguvu, Manispaa ina miradi mingi ya kufanya tukisema kila kitu
tusubirie Serikali ndugu zangu tutakuwa tunajichelewesha wenyewe,” Ameongeza
Waluse.
Miongoni
mwa Kata zilizotembelewa leo ni pamoja na Kata ya Luhungo Ujenzi wa Nyumba ya
Mwalimu na Ofisi ya Kata, Kata ya Mzinga ujenzi wa Shule ya Msingi Mpya , Kata ya Lukobe Ujenzi
wa Vyumba vya Madarasa, Kata ya Mkundi Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na eneo la
Mipango miji kwa ajili ya mwananchi kutaka kubadili matumizi ya kiwanja eneo la
Kilimanjaro, Kata ya Kingolwira Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi
Kingolwira pamoja na Ofisi ya Kata ya Kingolwira ambayo ipo katika hatua za
mwisho pamoja na Kata ya Uwanja wa Taifa katika Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Uhuru.
Ziara
hiyo itaendelea tena siku ya Jumanne Septemba 14 ikiwa na lengo la kupitia na
kubainai hali halisi ya miradi hiyo ili iweze kuongezewa nguvu na kukamilika
kwa wakati.
Post a Comment