Header Ads

DC MSULWA AWAGEUKIA WAVAMIZI WA VIWANJA VYA MICHEZO


Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Bakari msulwa, (katikati) , Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Rehema Bwasi, wakiwa na Vijana wa Jogging wakielekea Viwanja vya Gymkhana leo Septemba 26, 2020.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akizungumza na Vijana wa Mgambo pamoja na Jeshi la akiba waliojitokeza katika Viwanja vya Gymkhana kwenye majadiliano ya Wanamichezo .

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa Karatee Komfuu leo kwenye Viwanja vya Gymkhana.



Watumishi wa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika Viwanja vya Mashujaa tayari kwa mbio za kulekea Gymkhana.


Watumishi wa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika Viwanja vya Mashujaa tayari kwa mbio za kulekea Gymkhana.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Rehema Bwasi, katika kati akionesha tabasamu mbele ya Vijana wa Jogging leo.


Vijana wa Mgambo wakiweka viungo sawa kwenye Viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Morogoro.



Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dr Ikaji Rashid akionekana mwenye furaha baada ya kunyoosha  viungo vya mwili sawa kwenye Uwanja wa Gymkhana.


MKUU wa Wilaya ya Morogoro  amewataka watu wanaovamia maeneo ya viwanja vya michezo kukomesha tabia hiyo kwani inawanyima fursa vijana kushiriki kwenye michezo.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 26, 2020 kwenya Viwanja vya Michezo Gymkhana Manispaa ya Morogoro kwenye  Majadiliano ya kujadili Changamoto za Sanaa na Michezo  zinazo ikabili Wilaya ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Msulwa, amesema kuwa watu wanaovamia Viwanja vya michezo hawapaswi kuungwa mkono kwani wanawanyima ajira vijana pamoja na maeneo ya kufanyia mazoezi.

Msulwa,amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakivamia maeneo ya michezo na kujenga jambo ambalo linakwenda kinyume na matumizi yaliyopangwa na serikali hivyo vijana kushindwa kuendeleza vipaji vyao.

“Watu wenye tabia hii inabidi waiache kwani inadumaza azma ya serikali kuendeleza michezo mbalimbali hapa Wilayani kwetu na nchini kwa ujumla, hasa ikizingatiwa licha ya michezo kuwa ni burudani lakini pia inatoa fursa ya ajira hasa kwa vijana,” Amesema DC msulwa.

Amesema kuwa serikali imekuwa na mipango mbalimbali ya kuendeleza michezo ikiwa ni pamoja na kuwa na viwanja ambavyo vitawawezesha vijana kushiriki michezo hivyo watu wanaovamia na kujenga ni dhahiri wanakwamisha juhudi hizo.

“Tunaomba wadau wa michezo wahamasishe ujengwaji wa viwanja vya michezo, lakini amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kutoa taarifa za Kata ambazo zina viwanja vya michezo ikiwamo maeneo yaliyovamiwa na watu kuanza makazi ili hatua ziweze kuchukuliwa, lakini niseme kitu kimoja hawa Vijana wanamategemeo makubwa na Serikali yao niwaombe sana Wakurugenzi na Watendaji lazima tujikite katika kuibua vipaji vyao katika nyanja mbalimbali, tukifanya hizi tutatoa ajira na kuwapa uhuru Vijana hawa kuwa na maeoeno ya wazi ya kufanyia mazoezi pamoja na kuendeleza jitihada za serikali kuendeleza michezo hapa nchini” Ameongeza Msulwa.

Katika hatua nyengine, amesema lengo la majadiliano hayo ni 
kuwahamasisha vijana kushiriki michezo na sanaa jambo ambalo linatakiwa kupewa uzito wa hali ya juu kwa ajili ya kurudisha hadhi ya Mkoa wa Morogoro katika nyanja ya Michezo. 

Mwisho amesema Jumamosoi ijayo ya tarehe 03 Oktoba 2020, watakutana tena na Wanamichezo ili kutoa mrejesho wa yale waliyoyazungumza na kuwekeana mikakati ili kuyafanikisha na kuifanya Morogoro kuwa ya Viwango.
 
Ikumbukwe kwamba Majadiliano hayo yaliafuatiwa na Mbio za Vijana wa Jogging zilizoanzia katika Viwanja vya Mashujaa majira ya saa 7 asubuhi hadi katika Viwanja vya Ghymkhana ambapo katika mbio za Jogging iliongozwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema Bwasi , Watumishi wa Manispaa ya Morogoro, Jeshi la akiba na Migambo, Vijana wa Jogging mbalimbali, pamoja na Vijana wa Karate Komfuu ambao walishirikia katika majadiliano hayo.

Kwa upande wa mmoja wa wanamichezo, Sylivester Mokiwa, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya ubunifu wa kutaka kurudisha hadhi ya Mkoa wa Morogoro katika upande wa michezo.

'"Nichukue shukrani za dhati kumpingeza Mkuu wa Wilaya wetu, kwa kweli tulikuwa hatuna mategemeo kama tutakuja kuwa kitu kimoja lakini sauti zetu zimesikika na tunaona muelekeo mzuri wa Morogoro ya Viwango katika Michezo, niwaombe ndugu zangu tunapoitwa katika majadiliano kama haya tujitokeze kwa wingi, tumempata mtetezi wetu bila shaka sasa heshima ya Morogoro inarejea kwa kasi kubwa""Amesema Mokiwa.
 

KAULI MBIU : ""MOROGORO YA VIWANGO KATIKA MICHEZO  INAWEZEKANA""


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.