Header Ads

Mwenyekiti Machinga Manispaa Morogoro awataka Wanasiasa kuacha kutumia Vitambulisho vya wajasiriamali ndogondogo katika majukwaa kama agenda za kuwavuruga.

 




MWENYEKITI wa Machinga  Manispaa Morogoro , Faustine France, amewataka Wagombea kuacha tabia ya kunadi sera zao Majukwaani kwa kutumia ajenda ya Vitambulisho vya wajasiriamali ndogondogo Majukwaani ikiwa na lengo la kutaka kuwagawa wajasiriamali hao. 

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 24,2020  baada ya kusikia kauli zinazotolewa na Wagombea kwa kutumia kivuli Cha Vitambulisho vya wajasiriamali ndogondogo Jambo ambalo amelipinga vikali. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema ni wakati Sasa wa Wamachinga na Wajasiriamali wote kupinga kauli hizo kwani Vitambulisho hivyo wao ndio waliviomba na sio kwamba Rais ndiye alilazimisha Kama baadhi ya Wanasiasa wanavyosema.

 Amesema  kipindi Wanasiasa hao wapo bungeni wakati Wamachinga wananyanyaswa walikuwepo lakini walikuwa hawana dhana ya kweli ya kuwakomboa Machinga hao ambao walikuwa katika mateso makubwa.

 Amesema wanachotaka Sasa utaratibu huo uendelee kwani Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli, amekuwa mtetezi wa kweli na kuwafanya wajasiriamali ndogondogo kufanya kazi zao kwa Uhuru huku wakichangia Pato la Taifa kwa ajili ya maendeleo mengine . 

Amewataka Machinga wote nchi nzima wapaze Sauti ma kauli zinazotolewa na Wanasiasa kwani Zina lengo za kuwatenganisha na kuwakosesha amani wafanyabiashara kurudi katika utawala uliopita wa manyanyaso.

"Mimi Kama Mwenyekiti wa Machinga Manispaa Morogoro, na Makamu Mwenyekiti wa SHIUMA Tanzania, natoa wito kwa Machinga wote nchini wazipuuze kauli za Wanasiasa uchwara ambao Wana ufinyu wa mawazo wa kutaka kutugombabisha na Rais wetu ambae amekuwa amitupambania kwa kiasi kikubwa, awali hatukuwa na Maisha haya tunayoishi kwa Sasa, hao wanaopiga porojo awali walikuwa Viongozi lakini wametufanyia nini? Tulikuwa tunanyanyaswa wao wapo tuu , Sasa leo tumetulia na hali shwali wanaleta chokochoko, tusitumike Ndugu zangu, Kuna maisha baada ya uchaguzi Mambo ya siasa tuwaachie Wanasiasa lakini inapokuja ishu ya Kitaifa Kama hii yenye kugusa maisha ya Watu lazima tupaze Sauti, tunaungana na Mhe. Rais kwa Vitambulisho hivi vya wajasiriamali,  tunaomba wasio kuwa navyo wanunue maisha ya Sasa yamebadilika hatusumbuliwi Sasa kwanini tuwe mizoga? " Amesema Faustine.

"Nipende kuliweka wazi hili watu walifahamu, suala la sisi kupata vitambulisho lilichukua muda mrefu kuishawishi Serikali kutoka Ofisi ya TAMISEMI kupitia kwa aliyekuwa Waziri kipindi hicho mwaka 2017, tarehe 21 mwezi wa 5, na tulikaanae Ofisi ya Jengo la Mkapa House Jijini Dodoma mpaka analikubali pendekezo letu la kuiomba Serikali kwamba Machinga nao wawe wanachangia pato la Taifa jambo ambalo lilikuwa gumu kukubaliwa, kwahiyo ndugu zangu Viongozi wa Wamachinga nchi nzima pamoja na Wamachinga wote tumsaidie Mhe. Rais wetu kujibu maswali yanayotolewa na Wanasiasa sio kumuacha awe ana jibu mwenyewe hoja hizo sio sahihi Wanasiasa kutuchonganisha sisi na Serikali kwa sababu tuliyosaidiwa , hivyo kila Kiongozi wa Machinga Mikoani ajibu hoja hizi wanapotokea Wanasiasa wanazungumza suala la Vitambulisho kwa nia ya kutugombanisha na Serikali "Ameongeza Faustine.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.