Afisa Maendeleo ya
Jamii, Joyce Mugambi,(katikati) ambaye
alimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, ( kushoto) Mwenyekiti wa WAWATA Parokia ya Mtakatifu Patrick, Devotha
Ngatumbura wakiwa katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya Wakina Mama wa
Katoliki.
WANAWAKE Wakatoliki Parokia ya Mtakatifu Patrick Manispaa Morogoro, wamemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, kwa uongozi imara na thabiti, kwa ajili ya ustawi, mafao na maendeleo ya wananchi hususani katika kuwajali wanawake hao katika kufikia malengo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa WAWATA Parokia ya Mtakatifu Patrick ,wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wakina Mama iliyofanyika kwenye
kwenye Viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Patrick Septemba 27,2020.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa WAWATA Parokia ya Mtakatifu Patrick, Bi Devotha Ngatumbura amesema Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba, amekuwa kiongozi anaeguswa na mahangaiko ya watu, changamoto na magumu wanayokabiliana nayo kila kukicha.
""Kwakweli tunakila sababu ya kumpongeza Mkurugenzi wetu, tumeona tumuwalike japo amemtuma mwakilishi wake lakini tunaimani hata aliyekuwepo ni sawa na yeye yupo hapa, tumevutiwa na ushirikiano wake katika Ujenzi wa Kanisa la Mungu kama mchango wake mkubwa alioutoa katika Ukarabati wa Jiko la Seminari , hivyo tunampongeza kwa moyo wake wa upendo, huruma na furaha inayomwilishwa katika imani na kwamba, wao kama wanawake Wakatoliki wanapenda kumuunga mkono yeye pamoja na viongozi wote wa Kanisa ili kujenga ulimwengu unaojikita katika haki na maendeleo endelevu" Amesema Ngatumbura.
Amesema kuwa, Mkurugenzi ameonesha kuguswa sana na matatizo na changamoto zinazowakabili wanawake sehemu mbali mbali huku akisema ni wajibu wa wanawake pia kusimama kidete kulinda na kudumisha utu na heshima ya binadamu.
"Wanawake wanapaswa kuhusishwa kikamilifu katika mchakato wa majadiliano, ili waweze kuchangia ustawi na mafao ya wengi, kwa kuwapatia wanawake nafasi ya kutumua karama na mapaji yao, kwa mantiki hiyo imedhihirisha dhahiri kwa Mkurugenzi wetu jinsi anavyoguswa na matatizo ya wanawake jambo ambalo limewapa faraja kubwa na kuendelea kumpa ushirikiano na kumuombea kwa Mungu katika kipindi hiki ambapo amekuwa akikutana na majaribu ,mbalimbali katika nafasi yake" Ameongeza Ngatumbura.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii, Joyce Mugambi, ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , ameupongeza Uongozi wa WAWATA Parokia ya Kanisa la Mtakatifu Patrick kwa kutambua Mchango wa Mkurugenzi katika ustawi wa Kanisa kwa kumpatia heshima ya kuwa mgeni rasmi.
Mugambi, amesema kuwa WAWATA imejitahidi kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya umaskini miongoni mwa wanawake kwa kuwajengea uwezo kiuchumi na kijamii, ili aweze kujitegemea na kuzitegemeza familia zao.
Aidha ,amesema Kuanzia sasa Wanawake Wakatoliki wanahamasishwa kuwa ni chachu ya umoja na mshikamano wa dhati, kwa kutambua kwamba, wao ni makatekista wa kwanza katika kufundisha na kurithisha imani, maadili na tunu bora za maisha ya kijamii.
""Sisi Wakina Mama ndio chachu ya mabadiliko ya Watoto wetu , asilimia kubwa tumejisahau sana katika malezi, maadili yana momonyoka kwa Watoto wetu hii yote ni kukosa misingi imara ya Wazazi wao, hivyo Wakian Mama tunajukumu kubwa sana la kuhakikisha Watoto wetu wanakuwa na tabia nzuri na maadili ya kuridhisha , tusijisahau tuwafundishe nini wanatakiwa kukifanya ili iwasaidie katika maisha yao badala ya kuwaacha wakiharibikiwa wakiwa wadogo na kuwa hasara baadae" Amesema Mugambi.
Katika hatua nyengine,amewata
WAWATA Parokia ya Katoliki ya Mtakatifu Patrick, kuwa na ujasiri kwa kuielewa misingi sahihi ya
imani yao na hivyo kuitafsiri kwa vitendo katika medani mbali mbali za maisha,
daima wakisimama kidete kutetea Injili ya uhai, wakidumisha utu na maadili mema
pamoja na kuwa mstari wa mbele kuwainua
wanawake wenzao kutoka katika unyonge, umaskini na dhuluma, kama sehemu ya
mchakato unaopania kumkomboa mtu mzima: kiroho na kimwili.
Mwisho,amesema Jukumu ambalo liko mbele yao kwa sasa ni kuhakikisha kwamba, wanajikita katika malezi bora ya watoto na vijana, ili kulea na kustawisha amani ambayo inaendelea kuyumba siku hadi siku. Familia zioneshe upendo kwa vitendo ili Jamii iweze kuwatambua kuwa kweli ni wafuasi wa Kristo.
Post a Comment