KAMATI ZA SHULE ZATAKIWA KUFIKISHA TAARIFA KWA WAZAZI.
KAMATI za Shule zimetakiwa kufikisha tarifa kwa Wakati mara baada ya kujadili hoja zinazohusu Shule zai ili Wazazi waelewe na kuepusha migogoro ambayo inaweza kuporomosha viwango vya Ufaulu.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, Septemba 12,
2020 wakati wa mkutano wa hadhara wa Wazazi na Kamati ya Shule ya Msingi Chief
Albert iliyopo Manispaa ya Morogoro kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Freedom Square
SUA Mazimbu Compus Kufuatia Shule hiyo kuwa na mgogoro wa muda mrefu wa
takribani miaka 3 baina ya Kamati ya Shule pamoja na Wazazi.
Akizungumza
na Wazazi waliojitokeza katika Mkutano huo, DC Msulwa, amesema changamoto
nyingi zinazotokana na Wazazi ni Kamati za Shule kushindwa kufikisha taarifa
kwa haraka kwa Wazazi jambo ambalo linaleta migogoro na kufanya baadhi ya mambo
kutokwenda vizuri ikiwamo kuporomosha Viwango vya ufaulu shuleni.
DC
Msulwa, amesema lazima Kamati za shule
ziwe wazi kwa kutoa taarifa zile ambazo zimeamuliwa katika vikao halali vya
kamati ili wazazi waweze kufahamu na kuchangia.
“Migogoro
mingi ya Shule kutoka kwa Wazazi Kamati za shule zinachangia, hapa naamanisha
kwamba pengine Kamati hazikai vikao au hata kama zina kaa vikao basi hawa
Wazazi hawapati taarifa sahihi na kwa wakati, hoja zilizoletwa kwangu kupitia
Mkuu wa Mkoa kama mngekuwa mnawawafikishia taarifa hata tusingefikia huku,
niwaombe Kamati zijipange na zifuate utaratibu na miongozo ya Kamati zao,
Wazazi hawa wanahitaji taarifa, hawa ndio wenye Watoto mkiwa kimya hawawezi jua
nini kinaendelea, tukubaliane kwa pamoja sasa twende mbele hatutaki tena
kusikia migogoro ya Wazazi na Kamati , tunataka utaratibu ufauate ili wazazi
waweze kuchangia na hatimaye kupandisha Viwango vya ufaulu” Amesema DC Msulwa.
Aidha,
DC Msulwa, amezitaka Kamati za Shule zote zitengeneze mfumo mzuri wa kuweza
kushughulikia changanamoto za Shule zao na zipatiwe ufumbuzi na kuboresha
mawasilano baina ya Kamati na Wazazi.
Katika
hatua nyengine, DC Msulwa, amezitaka Kamati zote za Shule Wilaya ya Morogoro
ziwe na utaratibu wa kusoma mapato na matumizi kwa fedha zote zinazoingia katika
mzunguko wa Shule ili Wazazi waweze kutoa maoni yao.
“’Sio
suala la taarifa pekee lakini kitu ambacho nimekigundua ni kwamba Mapato na
matumizi hayasomwi, sasa twendeni katika mstari mmoja mapato yote na matumiz
Wazazi hawa wasomewe kwenye Vikao na viingie katika mihutasari ya vikao ili
wafahamu na kutoa maoni yao, mnaweza kuona taarifa zipo sahihi kweli lakini
hawa mkiwaficha ficha hawaelewi sasa tukifanya hivi hata hizi kero
zinazojitokeza sasa zitakwisha na tatakuwa kitu kimoja, huu sio muda wa migogoro,
Mhe. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anapeleka fedha kila mwezi kupitia
akaunti za shule za msingi kwa ajili ya kugharamia elimu kwa lengo la
kuwasaidia wananchi wanyonge lengo ni kunyanyua ufaulu tukianza minong’ono
tutachelewa kufika, niwaombe ndugu zangu tuwekeze katika elimu tusipokubali
kubadilika sisi wazazi hata watoto wetu hawawezi kubadilika, kitendo cha
kushtaki Kamati za Shule vikao
halali mlivyokubaliana sio jembo jema" ” Ameongeza DC Msulwa.
" Lakini nafikiria kuanzisha programu ambayo itanyanyua Viwango vya elimu katika Wilaya yetu, Kisarawe wenzetu walifanikiwa na sasa wanakwenda vizuri, hata sisi tukisema kila Mzazi aje na tofali moja au mbili tayari tushanyanyua darasa vyote vinawezekana kama sisi tukiamua,
Tuanze hapa tulipo kama wenzetu wameweza sisi tunashindwaje? Ameongeza DC Msulwa.
Mwisho amewataka Wazazi kwa kuhsirikiana na Kamati za Shule kuchukua jitihada nyingi sana za kuhakikisha ufaulu unaongezeka japo wapo watu wachache ambao ni waharibifu lakini watashughulikiwa ili maendeleo ya Elimu katika Wilaya ya Morogoro yaongezeke.
Katika
hatua nyingine, amezitaka Kamati za Shule ziweke pesa zote zinazoingia Shuleni zikae
huko na zisikae katika mikono ya watu ili kuleta usalama na uaminifu.
Kwa
upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema
yale yote waliyoyajadili katika kikao hicho watakwenda kuyafanyia kazi.
Amesema
lengo la kukutana ni kuona ni kwa namna gani Kamati za shule zinakwenda
kushirikiana na waalimu na wazazi ili kuboresha na kuinua viwango vya
ufaulu na kupata matokeo chanya katika Manispa ya Morogoro.
Post a Comment