MANISPAA YA MOROGORO YAUNGANA NA WADAU KUADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI.
Mkuu wa Masoko Manispaa ya Morogoro, Abdully Mkangwa, akizungumza na Waandishi wa habari leo Siku ya Usafi duniani.
Afisa Afya Manispaa ya Morogoro, Alex Roman,akizungumza na Waandishi wa habari leo Siku ya Usafi duniani.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Raleigh Tanzania, Abdallah Njayagha,akizungumza na Waandishi wa habari leo Siku ya Usafi duniani.
Usafi Soko la Manzese.
Wananchi wakifanya usafi Stendi ya Mabasi ya Dodoma nje ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro leo Septemba 19,2020 imeungana na wadau katika kusherehekea sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani katika Viwanja vya Soko la Manzese pamoja na Stendi ya Dododma nje kidogo ya Stendi ya Mabasi ya Msamvu.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Mkuu
wa Masoko Manispaa ya Morogoro, Abdully Mkangwa, amewashukuru wadau wa
Mazingira kwa juhudi za kuhakikisha mazingira yanatuzwa kwa hali zote.
Mkangwa,
amesema usafi wa leo umejumuisha Soko zima ikiwamo mifereji yote inayozunguka
Soko pamoja na mifereji iliyoko katika Barabara ya Kikundi inayounganisha magari ya SUA.
“”Kwa
ujumla wadau wameshirikiana vizuri na sisi, tunawaomba waendelee na moyo huo huo, kwa kweli hali ya usafi katika Masoko
yetu ya Manispaa ya Morogoro inaridhisha sana tofauti na mwanzo ambapo mambo yalikuwa sio mazunri lakini sasa tuna
wafanyakazi wengi na tuna vitendea kazi kama vile uwepo wa Mapipa ya kuhifadhia
taka yamerahisha kazi, kikubwa niwaombe Wananchi na Wafanyabiashara wa Masoko yote Manispaa waendelee
kutimiza jukumu la kufanya usafi huku wakituachia sisi jukumu la kuhakikisha tunafikisha hangaika kuzifikisha taka sehemu
husika ili Mji na Masoko yetu yawe safi na salama” Amesema Mkangwa.
Akitoa
salam na pongezi kwa wananchi, Afisa
Afya Manispaa ya Morogoro, Alex Roman, amewaomba wadau wa mazingira kuendelea kushirikiana na Manispaa ya Morogoro
katika kuweka Mji safi kwani wao wanatambua umuhimu wa wadau katika suala zima
la usafi.
''ninawaomba
Wadau wa Mazingira na Wananchi kwa ujumla kuhakikisha utunzwaji wa mazingira pamoja na
utunzwaji wa miti ya asili unazingatiwa, leo tunaadhimisha siku hii ,
tuhakikishe suala la usafi linakuwa ni endelevu, tunazo ratiba zetu kisheria ambazo kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tunafanya usafi, kwahiyo usafi unaanza
kwako mwenyewe kila mtu akibeba majukumu yake sisi Serikali, wadau pamoja na
Wananchi Mji wetu utaendelea kuwa safi na salama'' Amesema Alex.
Aidha,amebainisha athari ziletwazo na utunzwaji mbaya wa mazingira
kuwa ni pamoja na kutupa taka hovyo, kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni
mwa vyanzo vya maji , na kukata miti hovyo mambo ambayo yanaathiri sana
Mazingira.
Mwisho,
amewataka wananchi wotewa wa Manispaa ya
Morogoro, kuhakikisha wanazingatia agizo
la usafi wa mazingira kila jumamosi ya mwisho wa mwezi pamoja na kufanya usafi
katika Mazingira yao yanayowazunguka.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Raleigh Tanzania, Abdallah Njayagha ,
amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Taaisis za Serikali katika huduma za
Jamii mbalimbali kwani mpaka sasa wanahuduma za Vijana wanazozitoa kupitia
miradi mbalimbali katika baadhi ya Maeneo Manispaa ya Morogoro.
Miongoni
mwa huduma za Jamii wanazozitoa ni pamoja na mradi mkubwa wa Uwajibikaji wa
Jamii kupitia Vijana (Say) na mradi wa Kesho tutachelewa ambapo miradi yote
inatekelezwa ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Amesema
lengo la mradi huo ni kuleta hali ya ushawishi kwa jamii ili waweze kuwa wafuatiliaji wa miradi mbalimbali kwenye
jamii zao
Ikumbukwe
kwamba maadhisho haya hufanyika kila
tarehe 19/9 ya kila mwaka, lengo kuu
likiwa kuwakumbusha wananchi utunzwaji wa usafi wa mazingira kwa manufaa ya
vizazi vijavyo na kuwataka wadau na wananchi kusimama katika nafasi zao.
Maadhimisho haya yamehudhuriwa na wadau, wananchi, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali toka Manispaa.
Post a Comment