Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro aitaka Jamii kutoa taarifa kuhusu ukatili wa Kijinsia.
JAMII imetakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa juu ya vitendo hivyo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Wito huo umetolewa leo Juni 19,2020 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba, baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo hufanyika kila ifikapo juni 16 ya kila mwaka.
Akizungumza juu ya wito huo, Lukuba, amesema katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinakwisha , jamii inapaswa kutoa taarifa sehemu husika ili wahusika wachukuliwe hatua.
Lukuba, amesema baadhi ya wazazi na walezi , wamekuwa wakimaliza kimya kimya kesi zinazohusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia , jambo ambalo linasababisha watuhumiwa kurudia makosa hayo kwa watu wengine.
""Kila mmoja wenu analojukumu la kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi, madawati ya jinsia juu ya uwepo wa vitendo vya ukatili na si kukaa kimya kwani ili kuwa na jamii maendeleo endelevu ni lazima kuwekeza kwa watoto ambao ni Taiafa la kesho'"Amesema Lukuba.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa kipindi watoto wanapofanyiwa vitendo hivyo, wasisite kutoa taarifa kwa watu wao wa karibu wanaowaamini au katika klabu zao za shule.
Post a Comment