MANISPAA YA MOROGORO YATOA JUMLA YA MILIONI 517,800,000/= MIKOPO KWA VIKUNDI.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo akisoma hotuba katika sherehe ya kukabidhi hundi ya pesa kwa ajili ya Vikundi vya Mikopo.
Bajaji zilizotolewa leo na Manispaa ya Morogoro kwa vikundi vya mikopo ya uwezeshaji kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo (mbele ya Bajaji) pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro (nyuma ya Bajaji) wakizindua Bajaji zilizotolewa na Manispaa hiyo kwa ajili ya mkopo.
Katibu Tawla Wilaya ya Morogoro, Ruth John (kushoto) akiwa pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe (kulia) wakiwa ndani ya Bajaji zilzizotolewa mkopo leo na Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba akisakata mziki na Msanii wa Singeli Msaga Sumu leo katika shserehe ya kukabidhi hudni ya pesa kwa vikundi vya mikopo Manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo akikabidhi Mizinga ya nyuki 114 kwa Vijana.
Wananchi wakisakata muziki .
JUMLA
ya shilingi milioni 517,800,000/=
zimetolewa
kwa ajili ya mikopo ya uwezeshaji kwa vikundi 72, ikihusisha vikundi 44 vya
wanawake na vikundi 22 vya vijana pamoja
na Vikundi 6 vya Watu wenye Ulemavu.
Hatua
hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na
Sheria inayozitaka Halmashauri kutenga asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya
ndani kwa ajili mikopo ya uwezeshaji wa vikundi vya wanawake, vijana na watu
wenye ulemavu.
Akikabidhi
hundi za mikopo leoJuni 17, 2020 kwenye eneo la Shule ya Misingi Kiwanja cha Ndege kwa vikundi hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
, Mhe. Regina Chonjo,amesema fedha
walizokopeshwa zinapaswa kutumika kama chachu ya kuwaletea maendeleo.
Chonjo,
amesema kuwa fedha walizokopeshwa
wanapaswa kuzitumia katika malengo waliyoombea na siyo kupeleka katika matumizi
mengine kama vile starehe na anasa ambazo zitawafanya washindwe kurejesha.
Aidha,
amesema kuwa wanatakiwa kurejesha fedha hizo kwa wakati ili vikundi vingine vya
vijana , wanawake na walemavu waweze kukopeshwa kwa ajili ya kujiletea
maendeleo yao na jamii inayowazunguka.
‘”Nawapongeza
Wanavikudni wote kwa kukidhi vigezo vya kupewa mikopo na Manispaa ya Morogoro, Leo
nimewakabidhi hundi hii ya mfano mbele ya waandiashi wa habari, ni imani yangu
kuwa mtazitumia fedha hizi kwa malengo mliyojiwekea , hakikisheni mkopo huu
unawanufaisha watu wote bila ubaguzi , naamini hakuna hata kikudni kimoja
kitakachoniangusha , pia viongozi mliohudhuria hafla hii mtambue kuwa mmeingia
mkataba wa kupewa mkopo kwa niaba ya Vikundi vyenu , hivyo mfanye shughuli ya
pamoja kama mlivyoandika kwenye maandiko yenu ya mradi, lakini hatutaishia hapa
bali tutafanya ufuatiliaji wa kukagua utekelezaji wa miradi yenu kuona maendeleo
yenu” Amesema DC Chonjo.
Aidha
amesema Serikali ya awamu ya tano imekuwa pamoja sana na wananchi wanyonge hususani
Wajasiriamali na inawapenda sana na inathamini mchango mkubwa unaoletwa na
Wajasiriamali wadogowadogo katika kukuza pato la Taifa na ndio maana imeamua
kutoa mkopo bila riba.
‘”Ni
vye,ma mkajiuliza , ni wapi mtu unaweza kukopeshwa na kurejesha bila riba ?”
Tuutendee haki mkopo huu na kurejesha kwa wkati ili kusaidia na wengine kupata
fursa ya kukopo, tusimwangushe Rais wetu , yeye anatuonyesha kwa mfano : ni
jasiri , mchapa kazi na anatekeleza kwa vitendo na kutoa matokeo makubwa bila
woga, nasi hivyohivyo mkaitumie fursa hii ya mikopo mliyopewa kupata matokeo
makubwa” Ameongeza DC Chonjo.
Wakati
akikabidhi Bajaji 2 kwa vikundi hivyo, DC Chonjo, amesema wapo baadhi ya Viongozi ni
wabinafsi na wanatabia ya kuweka maslahi yao mbele huku akisema wakati Serikali
inapotaka kuwanunulia vikundi vifaa wao wanatafuta namna ya kuwarubuni ili
wanunue wao ambapo jambo hilo amesema halikubaliki.
Amesema
Serikali ya Rais John Pombe Magufuli siyo ya kununua vitu feki,vifaa vyote vipo
kwenye viwango vinavyotakiwa , vyenye viwango bora ikiwa na lengo la
kuhakikisha vinadumu kwa muda mrefu .
Pia
amewaagiza Maafisa Watendaji wa Kata na Maafisa Maendeleo ya Jamii wafuatilie
na kusimamia mikopo iliyotolewa kwa vikundi kwani pesa hizo ni kodi za wananchi
na ni lazima zirudishwe kwa wakati.
Mwisho
ameendelea kuwasisitizia wananchi kuchukua hatua na kufuata taratibu
zinazotolewa na wataalamu wa afya dhidi ya ugonjwa wa CORONA hususani watu
wanapokuwa katika shughuli za uzalishaji.
Kwa
upande wa aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya
Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, amesema kuwa mikopo waliyopewa haina riba kwa hiyo
wanapaswa kurejesha fedha kulinga na kiwango walichopata.
Kihanga,
amesema kuwa lengo la mikopo inayotolewa ni kuwakomboa vijana, wanawake na
walemavu kutoka umaskini na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Nchi.
Amesema
kuwa kikundi kitakachorejesha mkopo kwa
wakati kitapewa mkopo mwingine zaidi ya ule walioupata awali.
Naye
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema lengo la mfuko wa
maendeleo ya Wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu ni kutoa fursa kwa jamii ili
waweze kupata kwa urahisi mkopo usio na riba kwa wanavikundi kujidhamini
wenyewe.
Lukuba
amesema kuwa mikopo hiyo hutolewa ili kuongezea kujiendeleza kiuchumi na kuinua
hali za maisha ili kuendena na kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ya kufikia uchumi wa kati.
“Kwa
sasa Manispaa ya Morogoro imewapatia mikopo hii na nina imani kuwa mtaitumia
mikopo hii vizuri kuboresha biashara zenu na kurejesha kwa wakati ili kuwezesha
vikundi vingine viweze kukopa, kwa kufanya hivyo mtakuwa mmejenga imani na
kufungua milango ya kuongezewa mikopo na hata kutoa fursa kwa wadau wengine wa
maendeleo wanaojitokeza wenye nia ya kuwasaidia , wawasaidie kwa moyo” Amesema
Lukuba.
Akitoa
maelezo juu ya mikopo hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Bi
Enedy Mwanakatwe , amesema katika kipindi cha mwezi huu Juni Manispaa ya
Morogoro inatoa mkopo wenye thamani ya Shlingi Milioni 245,800,000.00 ambapo
kiasi cha shilingi milioni 110,900,000.00 kwa vikundi 44 vya Wanawake na
shilingi milioni 103,500,000.00 kwa vikundi vya Vijana na shilingi milioni
31,400,000.00 kwa vikundi 6 vya watu wenye ulemavu.
Mwanakatwe
amesema kiasi cha shilingi milioni 272,000,000.00 tayari zimetengwa kwenye
akaunti ya Wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu ambapo mchakato wa vikundi
vitakavyopatiwa mkopo huo upo katika hatua za mwisho.
“Vikundi
vinavyopewa mikopo ni vile ambavyo vimependekezwa na kamati ya maendeleo ya
kata na kufanyiwa uhakiki na kuonekana kuwa vinakidhi vigezo, lakini pia
tumevipa vipaumbele vikundi vinavyofanya shughuli za viwanda vidogodogo ambapo katika mkopo huu tumewanunulia Bajaji (3)
na Mizinga ya nyuki 114” Amesema Mwanakatwe.
Hadi
kufikia sasa Manispaa ya Morogoro imeshatoa
milioni 517,800,000/= kwenye mwaka huu wa fedha 2019/2020 ikiwa ni mikopo ya
vikundi mbalimbali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Post a Comment