Wenye maeneo wasiyoyaendeleza Manispaa Morogoro watakiwa kuyafanyia usafi.
Muonekano wa Makaburi ya Kola mara baada ya kufanyiwa usafi na Wananchi pamoja na timu ya mazingira manispaa .
MANISPAA ya Morogoro, imewataka Wananchi wote wa Manispaa ya
Morogoro ambao wanamiliki maeneo hawayaendelezi kuyafanyia usafi .
Kauli hiyo imetolewa
leo Juni 1, 2020, na Afisa
Mazingira Manispaa ya Morogoro, Samwel Subbi, katika kuelekea kilele cha
maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Subbi, amewataka wananchi
wa Manispaa ya Morogoro, waliotelekeza mashamba yao kwa muda mrefu na wenye maeneo ambayo hayaendelezi yapo wazi wasafishe
haraka na wahakikishe yanakuwa safi.
“ Tumeanza Kampeni yetu ya
usafi Manispaa ya Morogoro, lakini nipende kusema Manispaa haitakiwi kuwa na
Mashamba, hivyo wale waliotelekeza mashamba yao kwa muda mrefu na wenye maeneo ambayo hayaendelezi yapo wazi wasafishe
haraka na wahakikishe yanakuwa safi, la sivyo tutatumia sheria ili ya mipango miji ya kuwezakuyagawa
kwa watu wenye huitaji na wanaoweza
kuyaendeleza na kuwapiga fani wale ambao watashindwa kufuata sheria za usafi ’’ Amesema Subbi.
Aidha, amewataka viongozi
na watendaji wa Kata na wa vijiji waanze kuyabaini na kuorodhesha mashamba na
maeneo ya wazi yaliyotelekezwa kwamuda iwe rahisi kuyabaini yapo wapi na kwamuda gani yamebaki bila
kufanyiwa kazi.
Katika hatua nyengine, Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Winfred Kipako, amewatoa hofu wananchi kwamba zoezi hilo la kukagua maeneo yasiyoendelezwa kukagua usafi litatendeka kwa haki bila kupendelea na kumuonea mtu.Huku akiwataka viongozi na watendaji kuwa makini na waongozwe na uadilifu, uaminifu na uzalendo.Nayeyote atayeharibu zoezi hilo kwa masilahi binafsi atakuwa anathibitisha kuwa hasitahili kuwa kiongozi.
Kipako, amesema kuwa , Manispaa haijakurupuka kuanzisha Kampeni hiyo ya usafi na kuyabaini maeneo ambayo hayajaendelezwa huku akisema kuwa wamebaini kuwa mashamba mengi yaliyotelekezwa ni machafu hali inayosababisha kuwepo kwa vichaka .
"Ukiuliza unaambiwa shamba lilikuwa la babu yake,mwenyewe anaishi Dar au Iringa au nje ya eneo husika wakati huo ameliacha eneo lake nakugeuka pori linalotunza nguruwe, wanyama wakari, wadudu na hata kutengeneza mazaria ya Mbu na kusababisha ugonjwa wa Maralia , lakini nisema kama anaona yupo mbali na hawezi kulifanyia usafi eneo lake achukue aishi nalo hukohuko lakini likibaki Manispaa ya Morogoro bila kuendeleza tutawapiga faini na sheria za mipango miji zitatumika napengine hata kuyagawa kwa wenye uhitaji nayo” Amesema Kipako.
Mbali na onyo hilo, Kipako, amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro kutoa ushirikiano na kuwathamini watumishi wa serikali na kuacha mara moja tabia ya kuwazuia wasitimize na kutekeleza majukumu yao, Kwani baadhi yao wanatishia usalama wawatumishi wanapotekeleza majukumu yao.
Kwa upande wa Diwani wa
Kata ya Boma, Mhe. Amiri Nondo, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
kwa kubuni mpango mkakati wa kuanzisha Kampeni ya usafi huku akisema itasaidia
sana kuweka Manispaa safi na kuingia katika ushindani wa Halmashauri bora
katika suala la usafi Kitaifa.
Mhe. Nondo, amewaagiza
Watendaji wa Kata na Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waendelee
kuwafuatilia wale wenye maeneo ambayo hawayaendelezi ili kuwabaini na kama
watashindwa watachukuliwa hatua za kisheria ngazi ya Kata.
Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Hassan Malingo, amesema wamekuwa na utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo ya wazi licha ya kuwepo kwa kamapeni ya usafi.
“Tumehamasika zaidi baada ya kampeni hii, naaamini kwa jinsi tulivyojipanga tutalifanya zoezi hili kikamilifu ili kuipendezesha Manispaa yetu , kubwa tunawaomba wale ambao hawajitokeza wajitokeza baada ya wito mwengine “ Amesema Mhe. Malingo.
Katika hatua nyengine, Diwani wa Kata ya Kichangani,Mhe. Gilbert Mtafani, naye aliungana na Wananchi wake katika kuunga mkono Kampeni ya usafi Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Mtafani alipongeza sana jitihada za Mkurugenzi pamoja na timu ya wataalamu wa afya na mazingira wa Manispaa kwa kubuni mkakati ambao utaiwezesha Halmashauri kuingia katika nafasi za juu za usafi Kitaifa.
Naye Mtendaji wa Kata ya Mji Mkuu, Hamis Ally, amewapongeza Wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya usafi Manispaa ya Morogoro huku akiwaomba wananchi wanapoitwa katika jambo hilo wajitokeze zaidi ya hapo .
Ametoa wito kwa wanahci waendelee kujitokeza na kufanya usafi kuanzia katika maeneo wanayoishi na yanayowazunguka.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Bungo Kata ya Boma, Alex Kisitu, ametaka usafi huo uwe endelevu huku akitoa ahadi ya kushirikiana na Wazazi wote watahakikisha maeneo yote yanayozunguka Kata yao yanakuwa safi.
Post a Comment